Tanzania yashindwa kufurukuta mbele ya Uganda - EDUSPORTSTZ

Latest

Tanzania yashindwa kufurukuta mbele ya Uganda

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imeshindwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2023


Rodgers Mato ndiye aliyewapa Watanzania machungu leo akifunga bao katika dakika ya 90 baada ya Uganda kufanya shambulizi ya kushitukiza


Stars ilihitaji ushindi au hata alama moja ili kujiweka katika nafasi ya kufuzu lakini matokeo hayo yamefanya timu zote ziwe na nafasi


Stars imeendelea kusalia nafasi ya pili ikiwa na alama nne sawa na Uganda timu hizo zikiwa na uwiano sawa wa mabao ya kufunga na kufungwa


Niger inashika nafasi ya mwisho kundi F ikiwa na alama mbili wakati Algeria tayari imefuzu ikiongoza kundi F ikiwa na alama 12


Mchezo utakaofuata kwa Tanzania ni dhidi ya Niger, utapigwa Juni 2023 katika uwanja wa Benjamin MkapaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz