Rasmi: Kuziona Tanzania vs Uganda ni Buree - EDUSPORTSTZ

Latest

Rasmi: Kuziona Tanzania vs Uganda ni Buree


 Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Katika kutoa hamasa na kuunga mkono timu Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', ambayo kesho Jumanne itashuka uwnaja wa Benjamin Mkapa kuikabili Uganda katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Afcon 2023, Rais wa heshima Simba, Mohammed Dewji amenunua tiketi 5000


Aidha, kampuni ya Africarriers ambayo ni moja ya wafadhili wa klabu ya Simba, wamenunua tiketi 2000 wakati Azim Dewji na wafanyakazi wa kampuni yake wamenunua tiketi 1000


Afisa Habari wa TFF Clifford Mario Ndimbo ametangaza rasmi kuwa tiketi zote za Mzunguuko zimenunuliwa hivyo Watanzania wataruhusiwa kuingia bure


"Eneo la mzunguko tayari limeshajaa, kuanzia saa 6:00 mchana milango itakuwa wazi kwahiyo Mtanzania yoyote popote ulipo kuwahi kwako kufika ndio kuingia kwako. Kwenye eneo la mzunguko, kila mtanzania ana nafasi ya kuingia uwanjani kwakuwa tayari zimeshalipiwa"


"Kama tiketi zingekuwa chache tungetangaza utaratibu wa namna ya kupata lakini kwakuwa tayari zimenunuliwa zote basi milango ipo wazi kwa wote," alisema NdimboDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz