Nafasi za Ajira JWTZ Tanzania 2023
Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ limetangaza Nafasi za Kazi/Ajira kwa Watanzania mwaka 2023, wanahitajika Vijana Mbali Mbali, Elimu ni kuanzia Kidato cha Nne mpaka Chuo Kikuu, Deadline ni March 20, 2023.Sifa Za Mwombaji,Nafasi Za Kujiunga Na Jeshi,Utaratibu Wa Kutuma Maombi.
Nafasi za Ajira JWTZ Tanzania 2023 Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Leo Machi 9,2023 limetangaza nafasi za kujiunga na Jeshi hilo kwa vijana waliotumikia au kufanya mafunzo ya kujitolea katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa miaka miwili na kurejea nyumbani.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Uhusiano Luteni Kanali Gaudentius Ilonda akiwa Mjini Dodoma leo amesema kuwa “Vijana hawa walipata mafunzo ya JKT na walipofikisha miaka miwili walipewa vyeti baada ya kukosa nafasi ya kuandikishwa JWTZ au katika masuala mengine ya Ulinzi na Usalama Tanzania.
Taasisi/Vyombo vilirudishwa nyumbani lakini sasa nafasi imepatikana, naishukuru Serikali tumepata nafasi ya kuwaandikisha vijana hawa”
Ilonda ameongeza kuwa “Natambua katika matangazo haya ya kujiungana Jeshi kuna mwanya wa Matapeli utaibuka, Matapeli watapenda kutumia fursa hii, niwaombe Watanzania wote, Vijana na Wazazi wetu wasikubali Mtu kumwambia ‘nipigie simu kwamba nina fomu ya kujiunga’ kwanza hatutoi fomu”
“Mtu atakuambia ‘nina nafasi ya Kijana wako uliyoniomba sasa nafasi imepatikana, nina Afande ninamfahamu yupo Makao Makuu ya Jeshi ana nafasi zake nipe hela nikufikishe kwake’, ndio maana Afande mwenye nafasi hizo Jeshini hayupo nafasi zipo kwa haki sawa tutawapima kwa vigezo vyao”,
“Watanzania wasikubali kudanganyika hakuna njia ya mkato kwenye kupata hizi nafasi, katika hili la kupigiwa simu najua kwenye msafara wa mamba na kenge wapo kuna utapeli utaibuka, msikubali kutapeliwa”
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
NAFASI ZA KUJIUNGA NA JESHI
1.Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linatangaza nafasi za kujiunga na Jeshi kwa Vijana wa Kitanzania wenye elimu ya kuanzia Kidato cha Nne hadi Shahada ya Uzamili ambao wamemaliza Mkataba wa Mafunzo ya Kujitolea JKT na kurudishwa majumbani.
SIFA ZA MWOMBAJI
2.Vijana wa Kitanzania wenye nia ya kuandikishwa Jeshi wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
a.Awe raia wa Tanzania wa kuzaliwa mwenye Kitambulisho cha Taifa.
b.Awe na umri wa miaka 18 hadi 26 kwa wenye elimu ya Kidato cha Nne hadi Kidato cha Sita na umri usiozidi miaka 27 kwa wenye elimu ya Juu.
c.Awe na afya nzuri na akili timamu.
d.Awe Mtanzania mwenye tabia na nidhamu nzuri, hajapatikana na hatia ya makosa ya jinai Mahakamani na kufungwa.
e.Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate), vyeti vya Shule na vyeti vya Taaluma.
f.Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM).
g.Asiwe ameoa au kuolewa.
h.Awe amehitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mkataba wa kujitolea miaka miwili (2) na kutunukiwa cheti. Wale vijana wa JKT waliopo Makambini ambao wana sifa tayari, utaratibu wao wa kuwaandikisha unafanyika tofauti na vijana waliopo majumbani ambao tangazo hili linawahusu.
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
3.Maombi yote yaandikwe kwa mkono na yawasilishwe Makao Makuu ya Jeshi Dodoma kuanzia tarehe ya tangazo hili hadi tarehe 20 Machi, 2023 yakiwa na viambatisho vifuatavyo:-
a.Nakala ya Kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA.
b.Nakala ya cheti cha kuzaliwa, vyeti vya Shule na Chuo.
c.Nakala ya cheti cha JKT.
d.Namba ya simu ya mkononi ya mwombaji.
MAOMBI YATUMWE KWA ANUANI IFUATAVYO
4.a.Mkuu wa Utumishi,
Makao Makuu ya Jeshi,
Sanduku la Posta 194,
DODOMA, Tanzania.
b.Email: ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilianzishwa tarehe 01 Septemba 1964 kwa lengo la kulinda uhuru wa nchi na mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbali na lengo hilo, majukumu mengine ya msingi ya JWTZ ni pamoja na; Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Ulinzi wa Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuendesha Mafunzo na Mazoezi ya Kuwa Tayari Kupambana wakati wote. Kufundisha umma shughuli za Ulinzi wa Taifa.
Kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa majanga. Kukuza elimu na uzalishaji wa kujitegemea kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Kushiriki katika shughuli za Kimataifa za Ulinzi wa Amani.
Vijana wengi wamekuwa wakitamani kujiunga na JWTZ lakini hawajui njia sahihi wanazopaswa kuzipitia ili kuweza kutimiza ndoto zao ambapo hali hiyo inasababisha kuwepo kwa matapeli wengi.
Matapeli hao wanatumia kigezo cha watu kutojua kujiunga na JWTZ ili kuwatapeli wakisema wanaweza kuwasaidia. Mbali na hilo, vijana hao pia hawajui sifa za mtu anayeweza kukubalika kujiunga na JWTZ.
Wengi wamekata tamaa wakiamini hawana sifa za kufanya hivyo, na wengine wanatapeliwa wanapoahidiwa kusaidiwa wakati hawana sifa za kujiunga na JWTZ.
Kuna sifa Kuu 6 ambazo yeyote anayezitimiza ataweza kusajiliwa. Kuandikishwa kwa mtu wa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwenye sifa zifuatazo:
SIFA za kujiunga na JWTZ
- Kijana lazima awe raia wa Tanzania aliyezaliwa akiwa na umri wa miaka 18-26
- kuanzia kidato cha IV hadi kidato cha VI
- Kwa wale walio na elimu ya juu kufikia digrii, umri haupaswi kuzidi miaka 27
- Anapaswa kuwa na afya njema ya mwili na akili, tabia njema, nidhamu nzuri na lazima awe hajawahi kupatikana na hatia ya kosa la jinai au kushtakiwa Mahakamani na kufungwa gerezani
- Pamoja na kuwa na cheti halisi cha kuzaliwa, vyeti vya shule na taaluma.
- Pia awe hajawahi kutumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo na Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo na awe na cheti cha kutumikia JKT kwa miaka miwili”
Utaratibu wa kujiunga na JWTZ
Mtu yeyote ataandikishwa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa sifa zifuatazo: –
Awe raia wa Tanzania
Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe amefaulu..
Awe hajaoa/hajaolewa
Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25
Awe na tabia na mwenendo mzuri
Awe na akili timamu na afya nzuri
Masharti ya Utumishi
Askari atapewa nambari ya utumishi baada ya kufaulu mafunzo ya awali.
Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili miwili kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.
Maafisa
Bodi ya Uteuzi wa Maafisa (Officers Selection Board)
huwafanyia usaili Askari wenye elimu ya kidato cha sita na kuendelea toka Vikosini na Shule za Askari wapya (Recruitment Schools).
Watakaofaulu masailiano hayo hupewa hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet), na hupelekwa Chuoni (Tanzania Military Academy) kwa mafunzo ya Uafisa kwa muda wa mwaka mmoja.
- MSIMAMO Kundi D CAF Confederation Cup 2022-2023
- MSIMAMO Kundi C CAF Champions League 2022-2023
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili ya hatua ya 16 Bora Azam Sports Federation Cup 2023
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
The post Nafasi za Ajira JWTZ Tanzania 2023 appeared first on Nijuze Mpya.
from Michezo – Nijuze Mpya https://ift.tt/KySlLDf
via IFTTT
No comments:
Post a Comment