Messi huyoo afikisha Mabao 800 - EDUSPORTSTZ

Latest

Messi huyoo afikisha Mabao 800

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
 
Nyota wa Argentina aliyeshinda Kombe la Dunia, Lionel Messi aliliongoza Taifa lake kuifunga Panama 2-0 siku ya Alhamisi katika mechi ya kirafiki ambayo kimsingi ilikuwa kusherehekea ushindi wao wa Kombe la Dunia Desemba mwaka jana


Mabingwa hao wa dunia walitawala mchezo huo, hawakupata bao hadi dakika ya 78 pale Thiago Almada alipofunga bao baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Messi kugonga nguzo ya goli


Dakika kumi baadae, ilikuwa zamu ya Messi na akafunga bao la 800 la taaluma yake kwa mkwaju wa faulo. Sasa amefunga mabao 99 kwenye timu ya Taifa ya Argentina


Messi anakuwa mchezaji wa pili kuwahi kufikisha mabao 800 nyuma ya Ronaldo ambaye anashikilia rekodi ya muda wote ya kufunga mabao 830



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz