Yanga imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Geita Gold walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya 20 kupitia kwa Elias Maguli aliyemzidi maarifa mlinzi wa Yanga Dickson Job kabla kuukwamisha mpira kimiani
Matokeo Mtibwa sugar vs Simba February 11,2023
Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Yanga na kufanya mashambulizi mfululizo kwenye lango la Geita lakini mpaka mapumziko Wananchi walikuwa nyuma kwa bao 1-0
Mabadiliko aliyofanya kocha wa Yanga Nasreddine Nabi kwa kuwaingiza Metacha Mnata, Stephane Aziz Ki na Jesus Moloko nafasi za Djigui Diarra, Mudathir Yahya na Farid Mussa yalikuwa na faida kwa Yanga kwani Wananchi walifanya msako mkali kwenye lango la Geita Gold
Dakika tatu tu zilitosha wao kurejea mchezoni kupitia kwa Kennedy Musonda aliyefunga bao mahiri la kichwa kwenye dakika ya 48 kabla ya Clement Mzize kuongeza bao la pili kwenye dakika ya 50 akimalizia mpira uliotemwa na mlinda lango wa Geita Gold baada ya shuti la Musonda
Msumari wa tatu wa Yanga uliwekwa kimiani na Jesus Moloko kwenye dakika ya 70 baada ya pasi mahiri kutoka kwa Aziz Ki
Ni alama tatu ambazo zimeifanya Yanga ijiimarishe kileleni mwa msimamo wakifikisha alama 65 wakirudisha gap la alama nane dhidi ya Simba
Kimahesabu Yanga inahitaji kushinda mechi tatu zinazofuata (ukiwemo mchezo dhidi ya Simba) ili kutetea ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo
No comments:
Post a Comment