Ferguson na Arsene Wenger wafanyiwa jambo hili kubwa - EDUSPORTSTZ

Latest

Ferguson na Arsene Wenger wafanyiwa jambo hili kubwa

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 

Sir Alex Ferguson na Arsene Wenger ndio mameneja wa kwanza kuingizwa kwenye Jumba la Umaarufu la Premier League


Makocha hao wawili mashuhuri wanasifika kwa wakati wao wakiwa na Manchester United na Arsenal, ambapo walishinda mataji mengi


Ferguson alishinda mataji 13 ya Ligi ya Premia katika miongo mitatu, Vikombe vitano vya FA, Vikombe vinne vya Ligi na Ligi ya Mabingwa mara mbili huku Wenger akinyanyua mataji matatu ya Ligi Kuu na saba ya FA.


Wakati wao, Manchester United na Arsenal zilikuwa na upinzani wa aina yake. Timu hizo zilipokutana ilikuwa moja ya mechi kivutio katika ligi ya Premia


"Mameneja mashuhuri Sir Alex Ferguson na Arsene Wenger leo wameingizwa kwenye Ukumbi wa Umaarufu wa Ligi ya Premia," taarifa kutoka kwa shirika hilo ilisema.


"Wawili hao waliunda historia ya kushangaza na Manchester United na Arsenal, wakishinda mataji 16 ya Ligi Kuu ya Uingereza huku wakianzisha moja ya wapinzani maarufu katika historia ya Ligi"


"The Hall of Fame inatambua na kusherehekea watu ambao wana rekodi ya kipekee ya mafanikio na wametoa mchango mkubwa kwa Ligi Kuu tangu kuanzishwa kwake 1992. Ni heshima ya juu zaidi ya mtu binafsi iliyotolewa na Ligi"Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz