Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wananchi Yanga watakuwa miongoni mwa timu nane ambazo zitahusika katika droo ya robo fainali ya kombe la Shirikisho
Mechi za kuhitimisha makundi zinapigwa mwishoni mwa wiki hii Yanga ikitarajiwa kuondoka Dar leo kuifuata TP Mazembe kwa ajili ya mchezo utakaopigwa April 02 huko Lubumbashi pia Simba ni miongoni mwa timu nane zilizofuzu robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa ikimaliza kwenye nafasi ya pili kutoka kundi C
Mechi za kuhitimisha makundi zinapigwa mwishoni mwa wiki hii Simba ikimaliza mechi yake ya mwisho dhidi ya Raja Casablanca huko Morocco mchezo ukipigwa saa saba usiku wa kuamkia Jumamosi
Yanga imepania kumaliza kileleni mwa kundi D ili kuanzia mechi ya robo fainali ugenini na kisha kumalizia nyumbani huku
Simba ikiwa tayari kukutana na yeyote katika hatua ya robo fainali kwani hakuna timu nyepesi katika hatua hiyo
No comments:
Post a Comment