Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza imemfuta kazi Meneja Patrick Vieira baada ya kuiongoza kwa miezi 18.
Vieira ameondoka Palace baada ya michezo 12 bila ushindi katika mashindano yote, ushindi wake wa mwisho ukiwa dhidi ya Bournemouth kwenye mkesha wa Mwaka Mpya 2022
Palace walitupwa nje michuano ya FA katika raundi ya tatu dhidi ya Southampton inayoshika mkia kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, huku wakiporomoka hadi kufikia pointi tatu kwenye eneo la kushuka daraja
Mechi ya mwisho ya Vieira kuinoa Palace ilikuwa kupoteza 1-0 dhidi ya wapinzani wao Brighton, mchezo wa nne mfululizo ambapo klabu hiyo ya London kusini ilishindwa kufunga bao
No comments:
Post a Comment