Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wakati Ligi Kuu ya NBC imesimama kupisha kalenda ya mechi za kimataifa, Azam FC na KMC zinatarajia kukutana katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa Jumatatu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam
Taarifa iliyotolewa na Azam FC imesema baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya JKU ya Zanzibar, wameamua kujiimarisha kwa kuendelea kujipima nguvu.
Awali Azam walitarajia kujipima na vigogo wa Kenya, Gor Mahia lakini mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa ulivunjika kutokana na machafuko ya kisiasa yanayoendelea Kenya
Jana KMC waliifunga Dar City inayoshiriki Ligi ya Championship mabao 8-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam
Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam inakamata nafasi ya nne ikiwa na pointi 47 na katika hatua ya robo fainali ya Kombe la FA itacheza dhidi ya Mtibwa Sugar huku KMC yenyewe inapambana kujinusuru na hatari ya kushuka daraja
Post a Comment