VIDEO: Robertinho baada ya kupoteza vs Horoya AC CAF Champions League
Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema kuwa Klabu hiyo ilikosa bahati katika mchezo dhidi ya Horoya na hilo ndilo lilisababisha kupoteza ugenini kwa bao 1-0.
Robertinho ameongeza kuwa Simba imepoteza nafasi tatu za wazi ilizotengeneza ambazo zimetumika hata moja isingepoteza mchezo huo.
Akizungumzia mchezo ulivyokuwa, Robertinho alisema wenyeji Horoya walikuwa bora kipindi cha kwanza lakini Simba ilivyofanya mabadiliko kipindi cha pili iliishika mechi ingawa haikuzitumia nafasi ilizozipata.
“Nadhani hatukuwa na bahati, tumepata nafasi tatu za wazi lakini tumeshindwa kuzitumia. Wenzetu wamepata moja wameitumia na huo ndio mpira.
“Tunarudi nyumbani kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Raja Casablanca, naamini Wachezaji wetu wataitumia vizuri kupata Ushindi nyumbani,” alisema Robertinho.
Mchezo ujao dhidi ya Raja utapigwa February 18 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 Usiku.
- MSIMAMO Kundi C CAF Champions League 2022-2023
- MATOKEO Simba vs Horoya Athletic 11 February 2023 CAF Champions League
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- MATOKEO ya Kidato cha Nne 2022/2023
- RATIBA kamili ya hatua ya 16 Bora Azam Sports Federation Cup 2023
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
DONWLOAD NIJUZE TV HAPA SISI kwetu Michezo ndiyo Furaha YETU.
The post VIDEO: Robertinho baada ya kupoteza vs Horoya AC CAF Champions League appeared first on Nijuze Mpya.
No comments:
Post a Comment