Robertinho tuko tayari, mmoja kuikosa Raja Casablanca - EDUSPORTSTZ

Latest

Robertinho tuko tayari, mmoja kuikosa Raja Casablanca

Robertinho tuko tayari, mmoja kuikosa Raja Casablanca

Robertinho tuko tayari, mmoja kuikosa Raja Casablanca

Robertinho tuko tayari, mmoja kuikosa Raja Casablanca

Robertinho tuko tayari, mmoja kuikosa Raja Casablanca

Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema kuwa kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Raja Casablanca ambao utapigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuanzia saa 1:00 Usiku.

AKizungumza katika mkutano na wanahabari leo, Robertinho amesema kuwa anatambua wanakwenda kupambana na timu kubwa lakini hata Simba ni kubwa pia.

Robertinho tuko tayari mmoja kuikosa Raja Casablanca

Amesema jukumu la wachezaji wake ni kucheza kwa malengo na kufuata maelekezo, wanayo nafasi ya kushinda mchezo huo

“Ni mechi ngumu, Raja Casablanca ni timu kubwa kama tulivyo sisi, lakini tuna malengo. Kutokana na mipango yetu, tumejipanga kushinda”

“Tuna malengo ya kuvuka hatua ya makundi kwenda robo fainali, nusu fainali na hata kutwaa Ubingwa inawezekana. Nimewaandaa vijana wangu kucheza soka safi ambalo litaambatana na ushindi,” amesema Robertinho

Akizungumzia kukosekana kwa kiungo mkabaji Sadio Kanoute anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano, Robertinho amesema kukosekana kwa mchezaji huyo hakutaathiri kikosi chake

“Tutamkosa Sadio Kanoute lakini sina wasiwasi kwa sababu timu yangu ina wachezaji wengi. Hatuchezi kumtegemea mchezaji mmoja, nawaamini wachezaji 11 watakaonza watatupa matokeo ya ushindi”

 

The post Robertinho tuko tayari, mmoja kuikosa Raja Casablanca appeared first on Nijuze Mpya.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz