RAIS Samia aendelea kununua magoli ya Simba na Yanga
MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kununua kila bao litakalofungwa na Simba SC na Young Africans katika michuano ya CAF inaendelea.
Msigwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo amesema kuwa shilingi milioni tano kwa kila goli litakalofungwa na vilabu hivyo vyenye Makazi yake Jijini Dar es salaam itaendelea hadi mwisho wa Mashindano ya CAF.
Simba SC wapo Kundi C Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Raja Casablanca ya Morocco, Horoya AC ya Guinea na Vipers SC ya Uganda.
Young Africans wao wapo Kombe la Shirikisho pamoja na TP Mazembe ya DR Congo, US Monastir ya Tunisia na Real Bamako ya Mali.
Katika ahadi ya Kwanza ya Rais Samia, Simba ilizikosa fedha hizo baada ya kuambulia kichapo cha mabao 3-0 kutoka Raja Casablanca ya Morocco mwishoni mwa wiki Jijini Dar es salaam.
Kwa upande wa Young Africans wao walinufaika na ahadi hiyo baada ya kuichapa TP Mazembe ya DR Congo mabao 3-1 Jijini Dar es Salaam Jumapili.
Mabao ya Kennedy Musonda, Mudathir Yahya na Tuisila Kisinda yalitosha kuipa Yanga jumla ya Shilingi Milioni 15.
Kwenye mchezo huo bao la TP Mazembe lilifungwa na Alex Ngonga dakika ya 80.
Michezo ijayo itakuwa dhidi ya Vipers February 25 (CAF Champions League) kwa Simba SC ikisafiri hadi Uganda na dhidi ya Real Bamako February 26 (CAF Confederation Cup) kwa Yanga SC ikisafiri hadi Mali.
The post RAIS Samia aendelea kununua magoli ya Simba na Yanga appeared first on Nijuze Mpya.
from Michezo – Nijuze Mpya https://ift.tt/FExCsgQ
via IFTTT
No comments:
Post a Comment