Mambo matano muhimu kuelekea mchezo vs Horoya Athletic
Baada ya kupita takribani miezi minne kasoro wiki moja tangu Simba ilivyocheza mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika leo inashuka Uwanjani wa ugenini kucheza dhidi ya Horoya ya Guinea.
Hii ni mara ya kwanza Simba kukutana na Horoya AC katika historia yake, ikiwa haijawahi kucheza mchezo wowote nchini Guinea na hata mchezo wa kirafiki wowote dhidi ya Horoya Athletic Club.
Mchezo wa leo utakuwa wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kocha mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ kukiongoza kikosi sababu mechi zote nne za hatua ya awali timu ilikuwa chini ya kocha Juma Mgunda.
Mchezo wa leo pia utakuwa ni wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wachezaji Jean Baleke, Ismael Sawadogo na Mohamed Mussa ambao wamesajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili 2022/2023.
Safar ya Simba Sports Club Ligi ya Mabingwa Afrika ilianza hivi.
Mara ya mwisho kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa October 16 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo Simba iliibuka na Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Primeiro de Agosto ya Angola.
Katika mechi zote nne za hatua ya awali, ambazo Simba ilicheza iliibuka na Ushindi ikifunga mabao manane na kuruhusu bao moja pekee.
Matokeo ya mechi za hatua ya awali tumekuweka hapa chini.
September 10, 2022
FT Nyasa Big Bullets 0-2 Simba
(Moses Phiri, John Bocco)
September 18, 2022
FT Simba 2-0 Nyasa Big Bullets
(Moses Phiri yote)
October 09, 2022 FT Primeiro de Agosto 1-3 Simba
(Clatous Chama, Israel Patrick, Moses Phiri)
October 16, 2022
FT Simba 1-0 Primeiro de Agosto
(Moses Phiri)
Katika mechi nne za hatua ya awali Mshambuliaji Moses Phiri amefunga katika michezo yote huku akitupia kambani mabao matano.
Nahodha John Bocco, Clatous Chama na mlinzi Israel Patrick wamefunga bao moja kila mmoja.
- RATIBA kamili ya hatua ya 16 Bora Azam Sports Federation Cup 2023
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
DONWLOAD NIJUZE TV HAPA SISI kwetu Michezo ndiyo Furaha YETU.
The post Mambo matano muhimu kuelekea mchezo vs Horoya Athletic appeared first on Nijuze Mpya.
No comments:
Post a Comment