CAF Super Cup yazinduliwa, Bingwa kuvuna Mabilioni - EDUSPORTSTZ

Latest

CAF Super Cup yazinduliwa, Bingwa kuvuna Mabilioni

CAF Super Cup yazinduliwa, Bingwa kuvuna Mabilioni

CAF Super Cup yazinduliwa, Bingwa kuvuna Mabilioni

CAF Super Cup yazinduliwa, Bingwa kuvuna MabilioniCAF Super Cup yazinduliwa, Bingwa kuvuna Mabilioni, KUPITIA Mkutano wake Mkuu wa Kawaida wa 44, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limezindua Mashindano mapya ya Africa Super League yatakayoshirikisha Vilabu 24.

Vilabu hivyo vitatoka katika kanda tatu za kisoka Afrika huku kila ukanda ukitoa vilabu vinane (8) vitakavyounda Ligi hiyo itakayohusisha Mataifa 16 Barani Afrika.

CAF imetaja sababu Kuu ya kuanzisha Mashindano hayo kuwa ni kukuza thamani ya mpira wa Miguu Afrika kupitia uwekezaji, udhamini pamoja na mifuko ya maendeleo.

Africa Super League imetajwa kuwa itachezwa kwa kipindi cha miezi 10 kuanzia August hadi May kila mwaka na itakuwa na jumla ya michezo 197.

Fainali za mashindano hayo ambayo imepewa jina la SuperFinal itachezwa mwishoni mwa mwezi May katika Uwanja utakaoandaliwa kuwa na mfano wa Fainali za SuperBowl (Marekani).

CAF Super Cup yazinduliwaKatika mkutano huo, Rais wa CAF, Dkt. Patrick Motsepe amesema ndani ya miezi kadhaa ijayo, watatangaza mfumo mzima wa mashindano hayo na tarehe ambayo mashindano hayo yatatarajiwa kuanza.

Patrice Motsepe pia amesema kuwa Michuano ya Super Cup inayotarajiwa itazinufaisha Klabu zote zitakazoshiriki.

Akizungumza katika Mkutano wa mwaka wa CAF unaofanyika jijini Arusha, Motsepe amesema wanafahamu changamoto kubwa inayokwamisha maendeleo ya soka la Afrika ni fedha pamoja Changamoto ya Viwanja.

Amesema kupitia mashindano ya CAF Super Cup klabu zitapata fedha nyingi

Ukiacha viwanja tatizo kubwa kwa mpira wa Afrika ni fedha. Nimshukuru Rais wa FIFA Gianni Infantino kwa kutupatia wazo hili”

“Kupitia mashindano haya mapya ya CAF SUPER LEAGUE klabu zitapata fedha nyingi ambapo kwanza kila Klabu itapata dola milioni 2.5 kwaajili ya kusajili Wachezaji na Gharama za Michuano kama Usafiri na Hotel lakini pia Bingwa atapata dola Milioni 100.CAF Super Cup

Vilabu 24 Vinavyotarajwa kuwa vinaweza Kushiriki CAF Super League

1:Al Ahly ๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡ฌ
2:Zamalek๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡ฌ
3:Pyramid ๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡ฌ
4:Al Masry๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡ฌ
5:Wydad AC ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฆ
6:Raja Athletic ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฆ
7:RS Berkane ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฆ
8:Esperance ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ณ
9:Etoil Sportive Du Suhel ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ณ
10:Orlando Pirates ๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฆ
11:Kaizer Chiefs ๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฆ
12:Mamelodi Sundowns ๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฆ
13:JS Kabyile๐Ÿ‡ฉ๐Ÿ‡ฟ
14:CR Belouzidad ๐Ÿ‡ฉ๐Ÿ‡ฟ
15:E.S Setif ๐Ÿ‡ฉ๐Ÿ‡ฟ
16:TP Mazembe ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฉ
17:Horoya AC ๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ณ
18:SC Enyimba๐Ÿ‡ณ๐Ÿ‡ฌ
19:Petro de Luanda ๐Ÿ‡ฆ๐Ÿ‡ด
20:Simba SC ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
21:Asante Kotoko๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ญ
22:Al Hilal ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡ฉ
23:Asec Mimosas๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฎ
24:Coton Sport๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฒCAF Super Cup yazinduliwa

The post CAF Super Cup yazinduliwa, Bingwa kuvuna Mabilioni appeared first on Nijuze Mpya.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz