VIINGILIO Simba SC vs De Agosto October 16 2022 | CAF Champions League
Viingilio Simba vs De Agosto, Simba vs De Agosto CAF Champions League 2022, Viingilio vya mchezo Simba vs De Agosto Leo Jumapili, Viingilio Simba vs De Agosto October 16 2022, Viingilio Simba vs De Agosto CAF Champions League, Viingilio Simba SC dhidi De Agosto Leo, Simba vs De Agosto October 16 2022, Viingilio Simba vs De Agosto CAF Champions League, Viingilio Simba Sports Club vs De Agosto CAF CL.
KLABU ya Simba SC imerejea salama Jijini Dar es Salaam kutoka nchini Angola ilipokuwa kwaajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Premiero De Agosto ya nchini humo na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Baada ya kikosi kurejea wachezaji wamepewa mapumziko ya kwenda kukutana na familia zao kabla ya kuanza maandalizi mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumapili ijayo ya October 16, 2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es saa 10:00 Jioni.
Kesho kikosi hicho kitaanza mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena na Jumatano kitaingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo huo muhimu ambao Mshindi wa Jumla atatinga hatua ya Makundi moja kwa moja.
Katika hatua nyingine, Uongozi wa klabu hiyo hadharani Viingilio vya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Premiero De Agosto utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam saa 10:00 jioni.
Simba imesema kuwa kiingilio cha chini kwenye mchezo huo kitakuwa Tsh 3,000 ili kuwapa nafasi ya mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yao.
Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema kuwa wameweka viingilio rafiki ili kuwafanya mashabiki wa wapenzi wa Simba Sports Club kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao ili kufika hatua ya makundi kwa mara ya nne kwenye historia ya Klabu hiyo.
“Tumetangaza viingilio hivi mapema na rafiki ili kuwafanya mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi kuja kuishuhudia timu ikifuzu hatua ya makundi ambayo itakuwa ni mara ya nne,” amesema Ahmed.
Viingilio vilivyotajwa kwaajili ya mchezo huo ni;
Tsh 20,000 kwa VIP A, Tsh 15,000 VIP B, Tsh 10,000 VIP C, Tsh 5,000 kwa viti vya rangi ya Machungwa na Tsh 3,000 kwa Mzunguko.
-
WAFAHAMU Al Hilal Wapinzani wa Yanga CAF Champions League 2022/2023
-
MABADILIKO ya ratiba NBC Premier League 2022/2023
The post VIINGILIO Simba SC vs De Agosto October 16 2022 | CAF Champions League appeared first on Nijuze Mpya.
No comments:
Post a Comment