TAKWIMU Muhimu kuelekea Yanga SC vs Simba SC October 23 2022 - EDUSPORTSTZ

Latest

TAKWIMU Muhimu kuelekea Yanga SC vs Simba SC October 23 2022

TAKWIMU Muhimu kuelekea Yanga SC vs Simba SC October 23 2022

TAKWIMU Muhimu kuelekea Yanga SC vs Simba SC October 23 2022

Yanga vs Simba October 23 2022, Simba SC vs Yanga SC, Yanga vs Simba 23 October 2022, Simba Sports Club vs Young Africans SC 23 October 2022, Simba SC vs Yanga SC NBC Premier League, Yanga vs Simba Yanga Ligi Kuu, Yanga vs Simba watani wa Jadi, Matokeo Simba vs Yanga October 23 2022, Kariakoo Derby, Dar es Salaam Debry 23 October 2022, Derby ya Dar es Salaam Simba SC vs Yanga SC, Yanga vs Simba October 23 2022, Simba Sports Club vs Young Africans SC October 23 2022, Yanga SC vs Simba SC 23 October 2022.

TAKWIMU Muhimu kuelekea Yanga SC vs Simba SC October 23 2022

TAKWIMU Muhimu kuelekea Yanga SC vs Simba SC October 23 2022

BAADA ya tambo za hapa na pale kwa takribani wiki nzima, hatimaye siku yenyewe imewadia.

Ni Mchezo wa Derby ya Dar es Salaam/Kariakoo, Mchezo unaozikutanisha timu Kongwe hapa nchini maarufu kama mchezo wa watani wa Jadi kati ya Yanga dhidi ya Simba zote za Dar es Salaam, mchezo ambao utapigwa Leo Jumapili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Majira ya saa 11:00 Jioni.

Ni Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League 2022/2023), Matokeo ya mchezo huo ndiyo yataamua nani anaendelea kubaki kileleni mwa Msimamo wa Ligi, ambapo kwa sasa timu zote zina na alama 13, huku Simba ikiwa juu ya Msimamo kwa tofauti ya mabao tu.

Ni Mchezo muhimu sana kwa timu zote, huku Yanga ikitaka kurejesha furaha ya Mashabiki wake baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba wao wanahitaji kushinda mchezo huu ili kuendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi katika Msimu ambao Simba wamedhamiria kurudisha Ubingwa Mtaa wa Msimbazi.

Pia ni mechi ya kisasi kwa Simba ambayo itaingia dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii kwa kufungwa mabao 2-1

Simba chini ya kocha Juma Mgunda imeshinda kila mchezo uwe wa Mashindano au wa kirafiki, ambapo furaha ya Mwanasimba leo ni kuona timu yake inaibuka na Ushindi mnono dhidi ya Mtani.

Aidha takwimu zimeendelea kuibeba Yanga SC ikiwa na rekodi nzuri dhidi ya Watani zao katika Michezo ya karibu ambapo katika michezo mitano iliyopita Yanga imeshinda mitatu na kutoka sare michezo miwili.

Hata hivyo katika mechi za dabi, takwimu pekee hazitoshi kuihakikishia timu ushindi bali zinaweza kuwa chachu kwa timu kupambana ili kupata Matokeo.

Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na uhakika wa kumkosa Bernard Morrison anayetumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu, huku kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ akiwa kwenye hatihati kutokana na kurejea mazoezini siku chache zilizopita akitoka kuugua malaria

Kwa upande wa Simba SC itaendelea kuwakosa Shomari Kapombe na Jimmyson Mwanuke ambao bado wanaendelea kuuguza majeraha yao.

Nijuze Habari Kupitia nijuzehabari.co.tz tutakuleta moja kwa moja Matokeo ya mchezo huo unaotarajiwa kupigwa kesho Jumapili kuanzia saa 11:00 Jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Matokeo pia Nijuze Habari itakuletea Vikosi vyote vya Simba na Yanga mapema iwezekanavyo kuona Kikosi Cha Young Africans SC bofya HAPA.

Kuona Kikosi Cha Simba SC bofya HAPA na kuona Matokeo ya Mchezo huo bofya HAPA

The post TAKWIMU Muhimu kuelekea Yanga SC vs Simba SC October 23 2022 appeared first on Nijuze Mpya.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz