MGUNDA tuko tayari, wawili kuikosa Yanga October 23 2022 - EDUSPORTSTZ

Latest

MGUNDA tuko tayari, wawili kuikosa Yanga October 23 2022

MGUNDA tuko tayari, wawili kuikosa Yanga October 23 2022

MGUNDA tuko tayari, wawili kuikosa Yanga October 23 2022

MGUNDA tuko tayari, wawili kuikosa Yanga October 23 2022

MGUNDA tuko tayari, wawili kuikosa Yanga October 23 2022

KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Juma Mgunda, amesema kuwa maandalizi ya mchezo wa Derby dhidi ya Yanga SC yamekamilika na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri.

Mgunda amesema utakuwa mchezo mgumu wa ushindani lakini wamejipanga vizuri kuhakikisha wanashinda na kuchukua alama tatu muhimu.

Mgunda ameongeza kuwa katika mchezo huo Simba itaendelea kuwakosa Shomari Kapombe na Jimmyson Mwanuke ambao bado wanaendelea kuuguza majeraha yao.

“Mchezo utakuwa mgumu, lakini sisi tumejiandaa kuhakikisha tunashinda na kupata alama tatu huku tukicheza aina yetu ya mpira tulioizoea. Mechi ya Derby ni ngumu lakini tuko tayari,” amesema Mgunda.

Kwa upande wake Nahodha Msaidizi Mohamed Hussein, amesema kuwa kwa upande wao Wachezaji wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu kuhakikisha wanapata ushindi.

Zimbwe amesema kuwa wachezaji wanajua umuhimu wa mchezo huo na wamejipanga kuhakikisha wanawapa furaha Wanasimba kesho.

“Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari kwa mchezo, tunahitaji alama tatu kwa ajili ya kujiimarisha kileleni pia tuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Zimbwe Jr.

Nijuze Habari Kupitia nijuzehabari.co.tz tutakuleta moja kwa moja Matokeo ya mchezo huo unaotarajiwa kupigwa kesho Jumapili kuanzia saa 11:00 Jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Matokeo pia Nijuze Habari itakuletea Vikosi vyote vya Simba na Yanga mapema iwezekanavyo kuona Kikosi Cha Young Africans SC bofya HAPA.

Kuona Kikosi Cha Simba SC bofya HAPA na kuona Matokeo ya Mchezo huo bofya HAPA

The post MGUNDA tuko tayari, wawili kuikosa Yanga October 23 2022 appeared first on Nijuze Mpya.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz