MAANDALIZI ya Simba Kufuzu Makundi CAF Champions League 2022/2023 - EDUSPORTSTZ

Latest

MAANDALIZI ya Simba Kufuzu Makundi CAF Champions League 2022/2023

MAANDALIZI ya Simba Kufuzu Makundi CAF Champions League 2022/2023

MAANDALIZI ya Simba Kufuzu Makundi CAF Champions League 2022/2023

MAANDALIZI ya Simba Kufuzu Makundi CAF Champions League 2022/2023

MAANDALIZI ya Simba Kufuzu Makundi CAF Champions League 2022/2023

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa licha ya kufanikiwa kupata Ushindi mnono katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Premiero De Agosto bado Simba haijafuzu hivyo itapambana Jumapili kuhakikisha inafuzu hatua hiyo ya Makundi.

Ahmed amesema kuwa Msimu uliopita Klabu hiyo ilifanikiwa kushinda Ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana lakini ilipokuja nyumbani ikapoteza na kutolewa Mashindanoni kitu ambacho haitaki kijirudie.

Ahmed ameongeza kuwa Simba hahiitaji kufuzu hatua ya Makundi kwa kutegemea Ushindi ilioupata ugenini nchini Angola badala yake imejipanga kushinda nyumbani ili kuwapa furaha zaidi mashabiki na Wanachama Jumapili hii ya October 16 2022.

“Sisi tulishinda mechi ya kwanza ugenini lakini bado hatujafuzu. Mechi ya Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ndiyo utatupa tiketi ya kufuzu hatua ya makundi. Premiero De Agosto si timu mbaya tunapaswa kujipanga vilivyo.

“Tunataka kufuzu hatua ya makundi kwa kushinda nyumbani sio kutegemea ushindi tuliopata Angola wiki iliyopita. Tunataka kuwapa furaha mashabiki wetu ambao tunaamini watakuja kwa wingi uwanjani,” amesema Ahmed.

Katika hatua nyingine, Uongozi wa klabu hiyo mapema wiki hii uliweka hadharani Viingilio vya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Premiero De Agosto utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam saa 10:00 jioni.

Simba imesema kuwa kiingilio cha chini kwenye mchezo huo kitakuwa Tsh 3,000 ili kuwapa nafasi ya mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yao.

Viingilio vilivyotajwa kwaajili ya mchezo huo ni;

Tsh 20,000 kwa VIP A, Tsh 15,000 VIP B, Tsh 10,000 VIP C, Tsh 5,000 kwa viti vya rangi ya Machungwa na Tsh 3,000 kwa Mzunguko.

The post MAANDALIZI ya Simba Kufuzu Makundi CAF Champions League 2022/2023 appeared first on Nijuze Mpya.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz