KISINDA kuwepo au kutokuwepo vs Al Hilal CAF majibu yake haya hapa - EDUSPORTSTZ

Latest

KISINDA kuwepo au kutokuwepo vs Al Hilal CAF majibu yake haya hapa

KISINDA kuwepo au kutokuwepo vs Al Hilal CAF majibu yake haya hapa

KISINDA kuwepo au kutokuwepo vs Al Hilal CAF majibu yake haya hapa

KISINDA kuwepo au kutokuwepo vs Al Hilal CAF majibu yake haya hapa

TUISILA KISINDA YANGA SC

KUMEKUWA na Maswali Mengi miongoni mwa Mashabiki na Wanachama wa Klabu ya Young Africans SC kuhusiana na kiungo Mshambuliaji wao Tuisila Kisinda Kushiriki mchezo wa CAF Champions League dhidi ya Al Hilal Omduraman ya Sudan.

Klabu hiyo inathibitisha kuwa Tuisila Kisinda raia wa DRC Congo atakuwa miongoni mwa Wachezaji ambao Kocha Nabi anaweza kuwatumia katika mchezo huo unaotajiwa kuchezwa kesho October 08 2022 saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Dirisha la kwanza la CAF lilifungwa August 15, 2022 kwa Usajili wa hatua ya awali, hata hivyo CAF wakatoa tena fursa ya kuongeza Wachezaji wengine September 15, 2022 kwaajili ya hatua ya Kwanza.

Baada ya kukamilika kwa usajili wa Kisinda akichukua nafasi ya Lazalous Kambole ambaye aliachwa, Klabu hiyo iliongeza jina la Kisinda kwenye orodha hiyo ya wachezaji ambao watatumika kwenye hatua ya Kwanza.

Kutokana na hayo sasa ni rasmi Tuisila Kisinda atakuwa tayari kuwavaa Al Hilal Omduraman ya Sudan kwenye Mchezo huo ambao Mshindi wa Jumla atatinga hatua ya Makundi moja kwa moja.

The post KISINDA kuwepo au kutokuwepo vs Al Hilal CAF majibu yake haya hapa appeared first on Nijuze Mpya.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz