FEISAL Mchezaji Bora September NBC Premier League 2021/2022 - EDUSPORTSTZ

Latest

FEISAL Mchezaji Bora September NBC Premier League 2021/2022

FEISAL Mchezaji Bora September NBC Premier League 2021/2022

FEISAL Mchezaji Bora September NBC Premier League 2021/2022

KIUNGO wa Klabu ya Young Africans SC, Feisal Salum, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi September wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) huku Kocha Mkuu wa timu ya Namungo FC, Honour Janza akiibuka Kocha Bora wa mwezi huo.

FEISAL Mchezaji Bora September NBC Premier League 2021/2022

FEISAL Mchezaji Bora September NBC Premier League 2021/2022

Kikao cha Kamati ya Tuzo za TFF kilichokutana Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita kilimchagua Feisal, baada ya kuonesha kiwango kizuri kwa mwezi September na kutoa mchango mkubwa kwa klabu ya Yanga ikiwa ni pamoja na kufunga mabao mawili.

Feisal aliwashinda Mosses Phiri wa Simba SC na Reliants Lusajo
wa Namungo FC alioingia nao Fainali tuzo hiyo.

Feisal alikuwa na kiwango bora mwezi September, akifunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Azam FC na kuisaidia Yanga kupata sare ya 2-2.

Akizungumza na Feisal baada ya tuzo hiyo, alitoa pongezi zake kwa benchi la ufundi la Yanga, wachezaji wenzake na kuahidi kuwa tuzo hii imempa chachu ya Kwenda kupambana kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa, dhidi ya AL Hilal, utakaochezwa nchini Sudan Jumapili ya October 16, 2022

Honour Janza Kocha Bora September NBC Premier League 2022/2023

Honour Janza Kocha Bora September NBC Premier League 2022/2023

Kwa upande wa Honour Janza aliwashinda Charles Mkwasa wa Ruvu Shooting na Thiery Hitimana wa KMC
FC ambapo kwa mwezi huo Namungo iliifunga Ruvu Shooting bao 1-0, pia ikaifunga Coastal Union bao 1-0.

Smon Mwambe Meneja Bora wa Uwanja September NBC Premier League 2022/2023

Smon Mwambe Meneja Bora wa Uwanja September NBC Premier League 2022/2023

Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa uwanja wa Majaliwa, Lindi Smon Mwambe kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi September kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya Michezo pamoja na masuala yanayohusu Miundombinu Uwanjani.

The post FEISAL Mchezaji Bora September NBC Premier League 2021/2022 appeared first on Nijuze Mpya.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz