ZORAN afungashiwa virago Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

ZORAN afungashiwa virago Simba

ZORAN afungashiwa virago Simba

ZORAN afungashiwa virago Simba

ZORAN afungashiwa virago SimbaKLABU ya Simba SC imethibisha kufikia makubaliano ya pande zote mbili kuvunja mkataba na aliyekuwa Kocha Mkuu wake Zoran Maki raia wa Serbia mwenye umri wa miaka 60.

Taarifa kutoka Simba imesema kuwa pamoja na Zoran pia Klabu hiyo imefikia makubaliano ya kusitisha mikataba ya Kocha wa viungo Sbai Karim na Kocha wa makipa Mohammed Rachid.

Uongozi wa klabu ya Simba unawashukuru Makocha hao kwa mchango wao ndani ya klabu hiyo na inawatakia kila heri katika majukumu yao mapya.

Aidha Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya KMC FC Simba imesema kuwa kikosi hicho kitakua chini ya Kocha msaidizi Selemani Matola.

Taarifa imeenda mbali zaidi na kusema kuwa mchakato kutafuta makocha wapya watakaorithi nafasi hizo umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi karibini.

Zoran anaondoka Simba SC baada ya kudumu kwa siku 57 toka alipotambulishwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa Klabu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Msimbazi Jijini Dar es Salaam July 12,2022.

The post ZORAN afungashiwa virago Simba appeared first on Nijuze Mpya -| Pata Habari zote za Michezo kitaifa na Kimataifa, Tetesi na Usajili, Magazeti ya Michezo, Ratiba na Matokeo, Mahusiano Pamoja na Nafasi za Kazi.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz