SIMBA kucheza mechi mbili za Kirafiki Zanzibar, ratiba yake hii hapa.
Simba SC vs Malindi SC,Simba SC vs Kipanga FC,Simba Sports Club,Malindi SC,Simba Sports Club vs Kipanga FC,Simba vs Kipanga,Kipanga vs Simba,Malindi vs Simba,ratiba ya Simba vs Kipanga,ratiba ya Simba vs Malindi, Simba vs Kipanga, Simba vs Malindi.
KLABU ya Simba SC, imetua Visiwani Zanzibar kufuatia mwaliko kutoka Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) kwaajili ya kushiriki mechi za Kirafiki kipindi hiki Ligi ikiwa imesimama kupisha mechi za Kalenda ya FIFA.
Ikiwa Visiwani humo Simba inatajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Malindi SC na Kipanga FC.
Kikosi kimeondoka Jijini Dar es Salaam kikiwa na Wachezaji 21, benchi la Ufundi pamoja na baadhi ya viongozi.
Mchezo kwanza utakuwa dhidi ya Malindi SC Jumapili ya Septemba 25,2022 saa 2:15 usiku na mchezo dhidi wa pili dhidi ya Kipanga FC Jumatano ya September 28,2022.
Michezo yote miwili itapigwa kwenye Uwanja wa Amani uliopo Mjini Unguja Visiwani humo, Uwanja ambao una uwezo wa kubeba watu 15,000.
Baada ya michezo hiyo miwili Simba SC itarejea Jijini Dar es Salaam.
Ni Maandalizi ya mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Clube De Desportivo de Agosto ya nchini Angola utakaopigwa September 09, 2022.
Simba Sports Club ni timu ya Soka ya Tanzania iliyoanzishwa mwaka 1936 baada ya kutengana na timu nyingine ya Tanzania ijulikanayo kwa jina la Yanga SC na ilipewa jina la Queens kwa heshima ya Mtukufu Malkia wa Uingereza.
Kariakoo mtaa wa Msimbazi iliyopo Jijini Dar es Salaam nchini Tanzania ndipo nyumbani kwa klabu ya Simba Sports Club ambayo jina lake maarufu ni Simba SC.
Baada ya kujulikana kama Queens, klabu hiyo kisha ikawa Eagles, na hatimaye ikapewa jina la Sunderland na walibadilisha jina lao na kuwa Simba mwaka 1971.
Simba SC imeshinda mataji 21 ya Ligi na Vikombe vitano vya nyumbani, na imeshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mara nyingi.
Pia ni moja ya vilabu vikubwa Afrika Mashariki, wakiwa wametwaa Ubingwa wa Klabu Bingwa ya CECAFA mara sita.
Simba wakicheza mechi zao za nyumbani hutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Jijini Dar es Salaam.
Klabu hiyo ni mojawapo ya Klabu tajiri zaidi Afrika Mashariki, ikiwa na jumla ya bajeti ya Sh 6.1 Bilioni (sawa na $5.3 milioni) iliyozinduliwa kwa msimu wa 2019/2020.
Malindi Sport Club ni klabu ya soka ya Zanzibar yenye maskani yake Mjini Unguja.Ilianzishwa 1942 ni Klabu iliyopambwa zaidi Zanzibar.
Kwa miaka mingi walitawala Tanzania, kama Mabingwa wa Mashindano ya Zanzibar na Tanzania ya kikanda kuanzia mwaka 1989 hadi 1992.
Baada ya kutwaa mataji mengi ya Kitaifa na kikanda, timu hiyo ilianza kucheza Ligi Kuu ya Zanzibar mwaka 2004, baada ya Zanzibar kuwa mwanachama huru wa CAF, hivyo wanaiwakilisha Zanzibar katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika.
Kipanga Football Club , au kwa kifupi Kipanga ni klabu ya soka kutoka Afrika yenye maskani yake visiwani Zanzibar .
Kipanga FC inashiriki Ligi Kuu ya soka zanzibar, Ilianzishwa katika mji wa Kipanga visiwani Zanzibar na ikibaki kwenye kivuli cha timu kongwe katika eneo hilo, KMKM.
Timu hiyo ilishinda Ligi Kuu ya Zanzibar mwaka wa 2000 na Uwanja wa nyumbani ni Kipanga.
Kipanga wiki iliyopita ilifanikiwa kufuzu hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuwafunga Al Hilal Wau FC ya nchini Sudan.
The post SIMBA kucheza mechi mbili za Kirafiki Zanzibar, ratiba yake hii hapa. appeared first on Nijuze Mpya -| Pata Habari zote za Michezo kitaifa na Kimataifa, Tetesi na Usajili, Magazeti ya Michezo, Ratiba na Matokeo, Mahusiano Pamoja na Nafasi za Kazi.
No comments:
Post a Comment