WAGENI 12 ruksa kutumika Ligi Kuu 2022/2023
BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imetoa taarifa kuwa kwenye Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kilichoketi August 09, 2022 Jijini Arusha, kimepitisha Maboresho ya Kanuni za Ligi kuelekea msimu wa 2022/2023.
Moja kati ya maeneo yaliyoboreshwa ni idadi ya Wachezaji wa kigeni wanaoruhusiwa kusajiliwa na kutumika katika mchezo mmoja wa Ligi.
Kanuni mpya zimeruhusu Klabu kusajili Wachezaji wasiozidi 12 na kuwatumia wote yaani Wachezaji 12 (wote) katika mchezo mmoja.
Mabadiliko hayo yanaanza kutumika mara baada ya taarifa hii, ukiwemo mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Young African SC na Simba SC utakaouchezwa Jumamosi August 13, 2022.
Kwa mahesabu ya kawaida kwenye mchezo mmoja nafasi ya Wachezaji wazawa ni wachezaji 6 tu kwa idadi ya Wachezaji 18 wanaohusika kwenye Mchezo mmoja.
Bodi hiyo imesema kuwa klabu zina wajibu wa kufuata na kutekeleza masharti na taratibu zote za Usajili wa wachezaji wa kigeni zilizowekwa na TFF, zikiwemo sheria za nchi na taratibu za kufanya kazi nchini kabla hazijaanza kuwatumia Wachezaji hao.
Sekretarieti ya Bodi ya Ligi inaendelea na mchakato wa kuingiza maboresho katika kanuni za mwaka 2021 na punde zoezi hilo litakapokamilika, zitatumwa kwa wadau wote zikiwemo Klabu Shiriki.
- RATIBA Mechi Za Simba SC NBC Premier League 2022/2023
- KIKOSI Cha Yanga SC msimu wa 2022/2023
- RATIBA kamili Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/2023
- RATIBA Mechi za Yanga SC NBC Premier League 2022/2023
- KIKOSI Cha Simba SC msimu wa 2022/2023
- SIMBA, Yanga kuanzia hatua ya awali CAF Champions League 2022/2023
- SABABU zatajwa Simba SC kuanzia hatua ya awali CAF Champions League 2022/2023
- YANGA kwa Wasudan, SIMBA kwa Wamalawi, Droo ya CAF Champions League
- MABADILIKO ya muda, Simba vs Yanga ngao ya Jamii 2022, Viingilio vyawekwa wazi
- CAF Super Cup yazinduliwa, Bingwa kuvuna Mabilioni
- TAARIFA mpya kutoka Yanga SC August 10,2022
- TAARIFA mpya kutoka Simba SC August 11,2022
- MAGAZETI ya Tanzania Ijumaa August 12,2022
The post WAGENI 12 ruksa kutumika Ligi Kuu 2022/2023 appeared first on Nijuze Mpya -| Pata Habari zote za Michezo kitaifa na Kimataifa, Tetesi na Usajili, Magazeti ya Michezo, Ratiba na Matokeo, Mahusiano Pamoja na Nafasi za Kazi.
No comments:
Post a Comment