SIMBA kucheza Mechi 3 za Kirafiki kujiandaa na CAF na NBC Premier League - EDUSPORTSTZ

Latest

SIMBA kucheza Mechi 3 za Kirafiki kujiandaa na CAF na NBC Premier League

SIMBA kucheza Mechi 3 za Kirafiki kujiandaa na CAF na NBC Premier League

SIMBA kucheza Mechi 3 za Kirafiki kujiandaa na CAF na NBC Premier League

Simba kucheza Mechi tatu za Kirafiki, Simba kucheza mechi 3 za Kirafiki, Simba kucheza Michezo ya Kirafiki, Simba kucheza Michezo 3 ya Kirafiki, Simba vs Al Hilal ya Sudan, Simba SC vs Al Hilal, Al Hilal vs Simba SC, Al Hilal vs Simba, Al Hilal Simba Sports Club, Simba vs Asante Kotoko ya Ghana, Simba vs Asante Kotoko, Simba SC vs Asante Kotoko Simba Sports Club vs Asante Kotoko, Asante Kotoko vs Simba SC, Asante Kotoko vs Simba, Simba SC vs AS Arta Solar 7 ya Djibouti, Simba vs AS Arta Solar 7, Simba Sports Club vs AS Arta Solar 7, AS Arta Solar 7 vs Simba, AS Arta Solar 7 vs Simba SC, AS Arta Solar 7 vs Simba Sports Club.

SIMBA kucheza Mechi 3 za Kirafiki kujiandaa na CAF na NBC Premier LeagueKLABU ya Simba SC inatarajiwa kucheza Mechi tatu za Kimataifa za Kirafiki kujiandaa na Michezo ya CAF Champions League inayotajiwa kuanza September na Michezo ya Ligi Kuu ya NBC inayofuata.

Simba imepokea mwaliko maalumu kutoka Klabu ya Al Hilal ya Sudan Kushiriki Michuano Maalum ambayo itaanza kufanyika wiki ijayo.

Simba ikiwa nchini Sudan itacheza Mechi mbili dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana, August 28 na wenyeji Al Hilal August 31, mwaka huu.

Simba imepanga kuzitumia mechi hizo za Kimataifa kama sehemu ya maandalizi wakati Ligi Kuu ya NBC ikiwa imesimama kupisha mechi za kufuzu Fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Aidha Wachezaji tisa wa Simba walioitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayojiandaa na mchezo dhidi ya Uganda hawatakuwa sehemu ya safari hiyo.

Taarifa kutoka Simba imebainisha kuwa timu inatarajia kuondoka nchini Alhamisi alfajiri kuelekea nchini Sudan tayari kuwahi Mechi ya kwanza itakayopigwa August 28, dhidi ya Asante Kotoko.

Klabu ya Al Hilal imeendeleza Ushirikiano baina yao na Simba ambapo mwaka 2021 Simba iliwaalika katika Michuano ya Simba Super Cup ambayo iliandaliwa na Simba wenyewe.

Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Barbara Gonzalez ameishukuru Klabu ya Al Hilal kwa mwaliko huo ambao unaendeleza Ushirikiano na Mshikamano ambapo wenyeji wamegharamia kila kitu.

“Kipekee niwashukuru Al Hilal kwa mwaliko huu, licha ya kuongeza ushirikiano baina yetu lakini pia itakipa Mazoezi mazuri Kikosi chetu kipindi hiki Ligi ikiwa imesimama kwahiyo tunakuwa tumepata faida mara mbili,” amesema Barbara.

Baada ya kukamilika kwa Mashindano Kikosi Cha Simba kitarejea nchini na September 03,2022 Kitacheza Mechi nyingine ya Kirafiki ya kimataifa dhidi ya Mabingwa wa Djibouti, AS Arta Solar 7 mbaoo wapo kambini Jijini Dar es Salaam wakiwa wamesajili nyota kama Alexander Song na Solomon Kalou.Ratiba ya Mechi 3 za Kirafiki za Simba SC 2022

Mbali na Simba pia Klabu ya Azam FC inatajiwa kucheza mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki na AS Arta Solar 7 August 30 kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamanzi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Azam FC vs AS Arta Solar 7, AS Arta Solar 7 vs Azam Sports Club.

Mabingwa hao wa Djibout baada ya mchezo huo wa August 30 watacheza na Simba SC September 03,2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.Ratiba ya Mchezo wa Kirafiki wa Azam FC 2022

Katika hatua nyingine, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mdenmark, Kim Poulsen amemuongeza kiungo wa Azam FC, Tepsi Evans kwenye Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kuelekea mchezo wa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Uganda Jumapili hii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Tepsi Evans aitwa Timu ya Taifa ( Taifa Stars)Timu hizo zinatatajiwa kurudiana Septemba 03 kwenye Uwanja wa St. Mary’s Kitende Mjini Entebbe na mshindi wa jumla atafuzu Fainali za CHAN ambazo zitafanyika nchini Algeria kuanzia January 08 hadi 31,2023, Tanzania vs Uganda, Uganda vs Tanzania Kufuzu CHAN, Taifa Stars vs Uganda, Taifa Stars vs Uganda Kufuzu CHAN 2023 Algeria, Tanzania vs Uganda Kufuzu CHAN 2023 Algeria.

Simba kucheza Mechi tatu za Kirafiki, Simba kucheza mechi 3 za Kirafiki, Simba kucheza Michezo ya Kirafiki, Simba kucheza Michezo 3 ya Kirafiki, Simba vs Al Hilal ya Sudan, Simba SC vs Al Hilal, Al Hilal vs Simba SC, Al Hilal vs Simba, Al Hilal Simba Sports Club, Simba vs Asante Kotoko ya Ghana, Simba vs Asante Kotoko, Simba SC vs Asante Kotoko Simba Sports Club vs Asante Kotoko, Asante Kotoko vs Simba SC, Asante Kotoko vs Simba, Simba SC vs AS Arta Solar 7 ya Djibouti, Simba vs AS Arta Solar 7, Simba Sports Club vs AS Arta Solar 7, AS Arta Solar 7 vs Simba, AS Arta Solar 7 vs Simba SC, AS Arta Solar 7 vs Simba Sports Club.

The post SIMBA kucheza Mechi 3 za Kirafiki kujiandaa na CAF na NBC Premier League appeared first on Nijuze Mpya -| Pata Habari zote za Michezo kitaifa na Kimataifa, Tetesi na Usajili, Magazeti ya Michezo, Ratiba na Matokeo, Mahusiano Pamoja na Nafasi za Kazi.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz