Riwaya za kijasusi: Code X by Nelson Ntimba part 1 - EDUSPORTSTZ

Latest

Riwaya za kijasusi: Code X by Nelson Ntimba part 1

 

Riwaya za kijasusi: Code X by Nelson Ntimba part 1

RIWAYA: C.O.D.E.X
MTUNZI: Tariq Haji
SEASON 1
CONTACT: 0624065911
SEHEMU YA KWANZA
Allen James ni jina langu, ni dereva wa taxi katika jiji moja maarufu sana duniani Los Angels maarufu kama LA. Kama kawaida mapema vijana tunaingia kazini kutafuta mapeni. Nikiwa nasubiria abiria ghafla aliingia mtu na kunambia niondoe gari.
Nami nikifanya hivyo lakini nlipoangalia nyuma niligundua jamaa alikuwa akitoka damu na nlipojaribu kumwambia nimpeleke hospital alikataa na kunambia nimpeleke sehemu ambayo atakua salama. Nilijaribu kufikiria ni sehemu gani hiyo jibu lililokuja kichwani mwangu ilikuwa ni nyumbani kwangu.

Bila kuchelewa niliekea nnapo ishi, nilijaribu kumpatia huduma ya kwanza lakini alikuwa tayari kashapoteza damu nyingi sana hivyo uwezekano wa kuishi ulikuwa mdogo sana. Mwisho kabisa aliniita na kuninong'oneza CODE X, kisha akanipa kitu kama kitambulisho na picha, akanambia nisimtajie mtu yeyote neno lile hadi nitakapomuona mtu alienipa kwenye picha kisha hapo nae akaaga dunia. Nilibakia mdomo wazi nisijue nini cha kufanya kabisa.

Wakati nikiendelea kuwaza hivyo ghafla nikaskia gari zikifunga breki nje ya nyumba yangu. Nilipoangalia kupitia dirisha sikuamini macho yangu baada kuona watu waliovalia suti nyeusi huku wakiwa na silaha nzito. Mshale wa hatari uligonga kichwani mwangu na bila kufikiria nikajikuta nimenyanyuka na kuelekea ulipo mwili wa yule mtu. Nilichomoa bastola yake kwa ajili ya kujihami na haraka haraka nikapitia mlango wa nyuma.

Hata sijui ni kitu gani kilinipata lakini akili yangu iliniambia nielekee moja kwa moja New York City. Na bila kuchelewa niliingia kwenye gari yangu na safari ikaanza. Kwa bahati mbaya sana mmoja wao aliiona gari yangu na kuwashtua wenzake. Kivumbi kakaanza hapo, nilijitahidi kuwakimbia lakini wapi gari zao aina AUDI zilikuwa na uwezo mkubwa sana, hivyo walinifikia na kuanza kunigonga. Nlipoona mambo yanazidi kuwa magumu niliamua kuwapatisha ajali tu, nilifanikiw kwa gari kadhaa lakini bila mategemeo nilipgwa mzinga na gari yangu ikapinduka.Niliwahi kutoka kabla hawajanifikia na nikaanza kujibizana nao kwa risasi. Mwenyewe nilikuwa najishangaa maana sijawahi kuenda hata polisi lakini kwa jinsi nilivyokuwa nashambuliana nao ni kama nilikuwa nimebobea kwenye utumiaji wa silaha. Nilipohakikisha nimewamaliza nilichukua gari yao moja na safari ya kuekea New York ikaanza.
Safari ya kuelekea New York ikaanza, huku njia nzima nlikuwa nawaza uwezo ule wa kupigana nimetoa wapi maana tokea nipate fahamu zangu sikuwahi kujifunza ngumi. Lakini niliona bora niachane na mawazo hayo. Usiku ulinikuta njiani hivyo nikaona bora nitafute Motel nilale. Siku ya pili mapema niliendelea na safari yangu yenye sintofahamu nyingi, niliwasili New York mnamo saa nne na kidogo. Niliacha gari sehemu ya maegesho na kuanza kutembea kwa miguu lakini kwa umakini sana. Nilitembea mpaka kwenye hotel moja hivi na kuingia, maajabu nilioyakuta mapokezi yalizidi kunichanganya maana yule mschana aliekuwepo pale alinichamgamkia utasema labda tunajuana kwa muda mrefu sana. Bila hata kuongea kitu alinipa funguo ya chumba. Nilimshukuru na kuondoka huku moyoni nikijaimbia lazima nitafute muda niongee nae kwani anaonekana kujua mengi kuhusu mimi.


Nilifika chumbani kwangu kitu cha kwanza niliingia bafuni nikaoga maana uchovu ulikuwa ukinitafuna. Nilirudi ndani na kufungua kabati, macho yangu yalikutana na suti za bei mbaya tu. Nilichagua moja na kuvaa baada kuona nishapendeza nilikaa kitandani nikifiria mambo mengi yaliotokea siku ya nyuma. Wakati nikiwa mbali kwenye mawazo ghafla niliskia simu ikiita, niliangaza wapi ilipo na kwenda kuichukua. Nilipoipokea ukaingia ujumbe uliosema "kaa tayari ukisubiria maelekezo mengine". Ukaingia ujumbe mwengine "katika kabati kuna begi, litoe na fuata maelekezo utakayoyakuta".Nilifungua kabati na kutoa begi nikalifungua, nilikuta picha ya mzee mmoja nyuma ikiwa na ujumbe "chukua sniper iliokuwepo humu na uhakikishe huyu mtu anakwenda kuzimu". Niliiangalia ile sniper nikajikuta natabasamu, nilibeba lile begi na kuchukua ile simu kisha nikatoka. Nilipofika nje uliingia ujumbe mwengine "huyo mtu anapatiakana mji wa Alexandria na kazi ikamilike ndani ya masaa kumi na sita, chukua hiyo gari nyekundu mbele yako". Niliingia kwenye ile gari na safari ya kuelekea Alexandria ikaanza.
Nilipofika tu uliingia ujumbe ulionielekeza alipo, nilifika sehemu ya tukio na kupanda katika jengo moja refu kidogo lilikuwepo pembeni ya jumba alilokuepo huyo mlengwa. Nilipofika juu nilitoa sniper na kuiunga baada kukamilisha zoezi hilo nilijweka sehemu nzuri na kuanza kumtunga. Kwa msaada darubini ya sniper nilimuona vizuri na hapo nikafyetua risasi ilioingia kichwani na kusambaratisha ubongo. Sikuwa na haja ya kuichukua ile sniper, nilitoa bomu dogo na kulitega pale kisha nikaondoka. Iliripuka na Ushahidi ukapotea, nilipofika tu chini nilikaribishwa na risasi kadhaa hapo nikajuwa nimeshtukiwa.


Nilitoa bastola mbili ndogo na kuanza kujibu mashambulizi huku nikikoswa na risasi kadhaa. Kutoka kwa mlango huo ilikuwa haiwezekani nilirudi ndani na kuanza kutafuta mbinu za kutoka humo maana hata risasi zilikuwa zimeniishia. Mara walianza kuingia ndani,nilijibanza sehemu nikajisemea atakaepita kwanza ni halali yangu. Mara mmoja akapita nilimvuta ndani na kumvunja shingo, nikachukua bastola yake na kukimbia. Wakati nikiwa katika mapambano hayo uliingia ujumbe mwengine ukinitaka niondoke nchini marekani nielekee shanghai china. Nilifanikiwa kutoka nje na kuelekea ilipogari yangu na kutokomea, nilifanikiwa kuwatoroka. Moja kwa moja nilielekea uwanja wa ndege na kukata tiket ya ndege inayofuata kuelekea zangu Shanghai China. Muda wa kupanda ulifika na safari ya Shanghai ilianza na kwa jinsi nilivyokuwa nimechoka usungizi ulinichukua, usingizi uliombatana na ndoto mbaya za mateso ya hali ya juu sana.
*****
"jina lako nani" aliendelea kuniuliza uku akinipiga mgumi kadhaa za tumbo "Allen James" nilijibu lakini bado hakukubali. Mara nikamsikia akisema leteni mashine ya shot, haukupita muda ililetwa mashine hiyo. Aliiwasha na kutaka kunipiga shoti, ghafla nilishtuka kutoka usingizini huku jasho likinitoka, nilimuita muhudumu nikamwambia anipe kinywaji cha baridi baada hapo nilitulia nikiwaza ile ndoto. Kwa sababu ilikuwa ni ndoto tu nikaona bora niipoteze

.
Ndege iligusa ardhi ya Shanghai, nilishuka na kuelekea nje na nlipofika tu nje uliingia ujumbe "kuna macedes benz nyeupe kwenye maegesho, chukua hiyo gari na fuata maelekezo utakayoyakuta" niliangaza huku na huko mpaka nilipoiona na kuifuata. Niliingia kwenye gari hiyo, nilipowasha tu nikaskia sauti ya kike "karibu Shanghai Allen, fuata raman katika computer ya gari hii kufika katika hoteli uliopangiwa" baada hapo ile computer iliionyesha ramani na bila kupoteza muda nilianza safari ya kuelekea katika hiyo hoteli, ilinichukua dakika kumi kufika huko hotelini. Nilifika mapokezi nikataja jina, nikipewa funguo na kuelekezwa kilipokuwa chumba changu. Nilipofika chumbani niliingia chooni nikajimwagia maji na kubadilisha nguo. Wakati nikiwa nimepumzika ukaingia ujumbe "kwenye meza kuna picha na kisu, muue huyo mtu kwenye picha" nilsogea mezani na kuichukua picha. Dah macho yalinitoka kwasababu mlengwa wakati huu ni mwanamke. Nikajisemea moyono huyu mschana anabahati mbaya kweli na uzuri wote huu alokuwa nao leo anakwenda kuzimu. Nilishtuka kidogo na kujishangaa roho ile ya kikatili nimeitoa wapi.


Nilisubiri hadi usiku nikatoka kuelekea alipo huyo mschana na kwa msaada computer sikupata tabu sana kuijua nyumba yake. Basi nilifika lakini yeye hakuwepo hivyo niliingia ndani na kumsubiria, nusu saa baadae mlango ulifunguliwa, nilijibanza ukutani ili asije akaniona. "umekuja kuniua" aliongea yule mwanamke, nilijikuta nikimuuliza amejuaje kama nipo alkanijibu kuwa mambo yote ninayo yafanya yeye anajua. Nikamuuliza sasa alikuwa anajua kwanini aliamua kurudi, akaniambia kuwa anataka kunisaidia tu ili nitoke kwenye kifungo hicho cha utumwa.


Kidogo nilipowa baada kumsikia anataka kunisaidia maana hata mimi Mwenyewe nilikuwa sijijui tena. Aliniambia kuna kifaa nimewekewa kinachonindesha katika kufanya maamuzi na ndio maana kuuwa naona ni jambo sahihi kwangu. Nilimuuliza kama anaweza kukitoa akanijibu ndio lakini si wakati huo kwa sababu muda si mrefu tutavamiwa. Na kweli hatujakaa sawa tukaskia gari zikifunga breki. Aliniambia nimfate nami nikafanya hivyo, tulifanikiwa kutoka nje bila tabu na kwa kutumia usafiri wake tuliweza kuwaponyoka maadui zetu.


Kwa sababu yeye alikuwa mwenyeji nilimuachia awe kiongozi. Aliendesha gari kwa muda wa saa nzima, tulitoka nje ya mji wa Shanghai. Tulifika katika nyumba moja, hapo ndio ikawa mwisho wa safari yetu. Tulingia ndani, akasema tutapumzika usiku huo na siku itakayo fuata atanitoa hicho kitu.
Mapema siku iliyofuata alinifanyia operesheni ndogo na kukitoa. Alipokitoa tu nikapoteza fahamu. Nilikuja kushtuka nimo ndani ya chumba chenye kiza sana nilipojaribu kuinuka nilishindwa na nilipoangalia vizuri mikono yangu pamoja na miguu ilikuwa imefumgwa na ghafla taa zikawaka.
Dah nilijiona bwege kweli kudanganyika kirahisi kiasi kile, kwa mbali niliona watu wakija na nilipoangaza vizuri miongoni mwao ni yule mwanamke. Alipofika akaniuliza kama nimefurahia usingizi mzito, "kwani nimelala kwa muda gani?" nilimuuliza kwa shauku, akanijibu kuwa nimelala kwa muda wa masaa 72 kwa maneno mwengine nimelala kwa siku tatu. Baada maongezi hayo aliingia mtu wa makamo hivi, kwa kumkadiria ni kati ya miaka sabini au sabini na tano.
"kijana mimi sitak tusumbuwane" aliongea, "tusisumbuwane kivipi" ,nilihoji kwa sauti iliojaa hasira. Akanambia kuwa anahitaji password ya kufungua computer yenye siri za Project CODE X.


Nikamwambia kuwa mimi sifahamu chochote kuhusu jambo analoliongea, ghafla nilishtukia konde zito la tumbo lililonifanya nikohoe damu. Akarudia tena kuniambia jambo lile lile na mimi jibu langu lilikuwa lile kuwa sifaamu kitu chichite anachokiongea.
"inavoonekana kupata ukweli nitahitaji nitumie nguvu kidogo" aliongea yule mzee na kutoa ishara. Hapo waliingia jamaa watatu miraba minne na walionekana wapo kikazi zaidi. "Pigeni mpaka atakapo tupa kodi" aliongea yule mzee na kutoka. Basi wale washkaji walinisogelea na kunipa kipondo, nilijiapiza nikifanikiwa kutoka hai basi kila mmoja ataambulia kifo kibaya sana ambacho hajawahi kufikiria. Sikumbuki hata muda gani waliacha kunipiga lakini nilikuja kushtuka nimefungiwa chumbani. Kosa walilofanya ni kuamini kuwa mlango utanizuia kutoka na ndio maana hawakunifunga kama mwanzo.
BONGE LA KAZI TOKA KWA TARIQ.
ITAENDELEA KESHO HAPAHAPA.
HII NI SEASON ONE YA C.O.D.EX
IPO hadi Season 3.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz