RAIS FIFA ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA KILA HATUA - EDUSPORTSTZ

Latest

RAIS FIFA ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA KILA HATUA

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Dunia FIFA, Gianni Infantino amesema kuwa kukuza mpira wa Afrika kunahitaji ushirikiano mkubwa na kila mmoja ili kuweza kufikia mafanikio.

Inafantino aliwasili Tanzania Agosti 9 alipokelwa na mwenyeji wake ambaye ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) Wallace Karia pamoja na viongozi wa TFF ameweka wazi kuwa mpira wa Afrika unazidi kukua pamoja na dunia kiujumla.

“Tunahitaji kukuza mpira kwa kuanzia kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa, kuwa na timu imara za taifa ambazo zitaweza kufanya kila mmoja kuweza kuona matokeo ya kile ambacho anakifanya.

“Kwenye hayo tunahitaji makubaliano mazuri kwenye kila jambo na kushirikiana hatua kwa hatua,CAF na FIFA wote tuna kazi moja ya kufanya ili kuweza kuendelea kufikia kile ambacho tunakihitaji.

“Wanachama wote ambao tumeshiriki mkutano wa leo bado tuna kazi ya kuendelea kuyafanya yote kwa vitendo hasa ukizingatia bado tuna safari kuweza kufikia mafanikio,”.

Leo Arusha mkutano mkuu wa FIFA unafanyika Arusha huku ukiwa umewakutanisha wanachama wote wa FIFA.

The post RAIS FIFA ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA KILA HATUA appeared first on Saleh Jembe.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz