KUMUONA AZIZ KI,MORRISON,OKWA BUKU TANO - EDUSPORTSTZ

Latest

KUMUONA AZIZ KI,MORRISON,OKWA BUKU TANO

KUELEKEA kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa viingilio vimewekwa wazi leo Agosti 10,2022.

Mastaa ambao wanatarajia kuweza kucheza mchezo huo ni pamoja na Aziz KI,Bernard Morrison kutoka Yanga,Nelson Okwa, Victor Ackpan wa Simba.

Ni 5,000 kwa mzunguko kwenye viti vya kijani na bluu,kwa upande wa viti vya machungwa ni 7,000.

Kwa upande wa VIP C kiingilio ni 15,000,VIP B ni 20,000 na VIP A ni 30,000.

Yanga wanatetea taji hilo ambapo waliweza kushinda bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mtupiaji wa bao hilo walipokutana Uwanja wa Mkapa alikuwa ni Fiston Mayele aliyeweza kumtungua Aishi Manula.

The post KUMUONA AZIZ KI,MORRISON,OKWA BUKU TANO appeared first on Saleh Jembe.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz