DABI YAO YA KWANZA MASTAA HAWA WA SIMBA - EDUSPORTSTZ

Latest

DABI YAO YA KWANZA MASTAA HAWA WA SIMBA

AGOSTI 13 Uwanja wa Mkapa unatarajiwa kuchezwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga v Simba kuna nyota ambao itakuwa ni dabi yao ya kwanza.

Chini ya Zoran Maki wachezaji hao ni pamoja na Moses Phiri aliibuka Simba akitokea Zanaco.

Pia yupo Nassoro Kapama mzawa kutoka ndani ya Kagera Sugar.

Habib Kyombo mzawa kutoka Mbeya Kwanza,Victor Acpan ingizo jipya kutoka Coastal Union yeye ni raia wa Nigeria.

Nelson Okwa ni ingizo jipya kutoka Rivers United,Augustine Okra kutoka Bechem United,Mohamed Outtara kutoka Al Hilal ya Sudan,Dejan Georgijevic kutoka Domzale hawa wanatarajiwa kukaribishwa Uwanja wa Mkapa na mchezo wa Ngao ya Jamii.

Waliweza kuanza kuona joto ya mashabiki Agosti 8 kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya St George hivyo wana kazi nyingine tena.

The post DABI YAO YA KWANZA MASTAA HAWA WA SIMBA appeared first on Saleh Jembe.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz