KLABU ya Azam FC imetambulisha Mspaniola, Dani Cadena kuwa kocha mpya wa makipa kuelekea msimu ujao, huo ukiwa ni mkakati wa kurejesha makali ya timu.
Cadena ni kocha wa zamani wa makipa wa klabu za Ligi Kuu Hispania, ijulikanayo kama La Liga za Sevilla na Real Betis, ambaye pia ameshafanya kazi nchini China na Asaudi Arabia akiwa na uzoefu mkubwa na elimu ya juu ya Shirikisho la Soka la Ulaya UEFA.
Kocha huyo ametambulishwa siku moja na wachezaji wawili wapya, viungo washambuliaji kutoka Ivory Coast, Tape Edinho na Kipre Junior Zunon kutoka Sol FC na Tape Edinho kutoka ES Bafing zote za kwao, ambao wote wamesaini mkataba wa miaka mitatu kila mmoja.
No comments:
Post a Comment