KLABU ya Chelsea inajiandaa kutuma ofay a kuinasa saini ya kinda wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno Matheus Nunes mwenye umri wa miaka 23 anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji.
Inakadiriwa Chelsea wanajiandaa kutuma ofay a paundi milioni 45 ikiwa na nyongeza ya paundi milioni 5 ambayo itatokana na vipengele vya mkataba.
Nunes amekuwa na msimu mzuri akicheza kama kiungo mshambuliaji akiisaidia Sporting Lisbon kufunga jumla ya mabao 4 pamoja na pasi 5 za mabao katika msimu uliomalizika wa 2021/2022.
Hadi sasa Chelsea ni miongoni mwa timu tatu katika Ligi Kuu ya Uingereza ambazo hazijafanikiwa kusajili mchezaji hata mmoja hali inayopelekea mashabiki wake kuwa na wasiwasi juu ya utawala mpya chini ya umiliki wa Kampuni ya Clearlake na Todd Boehly.
Tayari klabu hiyo ya Chelsea imehusishwa na nyota wengi akiwemo Cristiano Ronaldo, Neymar Jr, Jules Kounde, Kalidou Koulibaly na nyota wengine wengi.
The post Chelsea Kutuma Ofa ya Kumnasa kinda wa Ureno Kutoka Sporting Lisbon appeared first on Global Publishers.
No comments:
Post a Comment