KLABU ya Yanga imefanikiwa kukusanya kiasi cha Bilioni 1.7 ndani ya kipindi cha miezi sita kutokana na malipo ya uandikishaji upya wa wanachama wake katika mfumo wa Kidijitali.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kilinet, Mohammed Saleh kutoka kampuni hiyo iliyopewa zabuni ya kuendesha zoezi hilo.
Saleh amesema kwamba mikoa inayoongoza kwa Usajili wa Wanachama kwenye mfumo huo wa Usajili wa Kidigitali ni Dar es Salaam wanachama 12,124, Mwanza 1,982, Mbeya 1,655, Dodoma 1,521, Morogoro 1,410 na Pwani 1,341.
“Ndani ya kipindi cha miezi 6 tumeweza kusajili Wanachama 34,650 na kukusanya mapato ya Tshs Bilioni 1.07,” amesema Saleh katika mkutano na Waandishi wa Habari leo Dar es Salaam.
Msemaji wa klabu, Haji Manara alisema Hatua inayofuata ni Kadi za Mashabiki, Mshabiki atakayetambulika Hatua inayofuata ni Kadi za Mashabiki, Mshabiki ambao kila mmoja atatakiwa kulipa Ada ya Sh 17,000, itakayomuwezesha kupatiwa Kadi ambayo ataitumia pia kuingia Uwanjani na kupata punguzo la Bidhaa mbalimbali za Yanga SC na maduka ya GSM washirika wa, klabu hiyo.
Naye Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mazingisa amesema kwamba anajivunia nafasi hiyo ndani ya Yanga kutokana na walivyovyofanikiwa kwenye zoezi la Usajili wa Kidigitali kwa kushirikiana na Kampuni ya Kilinet Africa.
No comments:
Post a Comment