Watu 130 Wauawa na Wanamgambo wa Kiislamu Nchini Mali Eneo la Sahel-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Watu 130 Wauawa na Wanamgambo wa Kiislamu Nchini Mali Eneo la Sahel-Michezoni leo

Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kiislamu waliua zaidi ya raia 130 mwishoni mwa juma katika miji jirani ya katikati mwa Mali, ikiwa ni mauaji ya hivi karibuni katika eneo hilo la Sahel lenye mzozo.

 

Maafisa wa eneo hilo wameripoti matukio ya mauaji ya kiholela yaliyofanywa na watu wenye silaha huko Diallassagou na miji miwili jirani katika eneo la Bankass, eneo la Sahel ambalo limekuwa lenye machafuko kwa muda mrefu.

 

“Walichoma pia vibanda, nyumba na kuiba ng’ombe,” amesema afisa wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu za kiusalama.

 

Yeye na afisa mwingine ambao wote wawili walikimbia kijiji chao, wamesema hesabu ya watu waliouawa ilikuwa ikiendelea Jumatatu.

 

Nouhoum Togo, afisa wa mji wa Bankass, mji mkubwa katika eneo hilo, amesema idadi ya waliouawa ni kubwa kuliko ile ya watu 132 iliyotangazwa na serikali, ambayo iliwashtumu wanamgambo wa kiislamu washirika wa Al-Qaeda kwa mauaji hayo.

MORRISON AWAOMBA SIMBA AKACHEZE YANGA, KUNA MIDO HUKO IMEITAJA SIMBA | KROSI DONGO

The post Watu 130 Wauawa na Wanamgambo wa Kiislamu Nchini Mali Eneo la Sahel appeared first on Global Publishers.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz