Watu watatu wamefariki na wengine saba wamejeruhiwa katika ajali ya basi la Zubery iliyotokea katika barabara ya ya Mwanza - Shinyanga katika eneo la Mwigumbi.
Taarifa zinaeleza kuwa Basi hilo liligonga Ukingo wa Daraja na kutumbukia bondeni na kusababisha vifi hivyo ambapo mmoja kati ya waliofariki ni dereva wa basi hilo aliyefahamika kwa jina la Hamza Katima.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, George Kyando amesema taarifa za awali zinaonesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Dereva wa Basi hilo kupata tatizo la kiafya akiwa safarini.
Polisi wametioa wito kwa madereva kuangalia afya zao mara kwa mara kabla ya kuanza safari ili kuepusha matukio kama hayo kutokea
No comments:
Post a Comment