SIMBA SC wametoka nyuma na kushinda 3-1 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
KMC walitangulia na bao la Hassan Kabunda dakika ya 41, kabla ya Simba kutoka nyuma kwa mabao ya Kibu Dennis dakika ya 51, Msenegal, Pape Sakho dakika ya 62 na beki Mkongo, Henock Inonga dakika ya 65.
Kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi 57, ingawa kushika nafasi ile ile, ya pili ikizidiwa pointi 10 na mabingwa tayari, Yanga baada ya wote kucheza mechi 27.
KMC baada ya kichapo hicho inabaki na pointi zake 32 za mechi 27 ikishukia nafasi ya 10 kutoka ya tisa.
No comments:
Post a Comment