Simba Wafunguka Tetesi za Kumsajili Ntibanzokiza ‘Saido’, Watangaza Mipango Mipya-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba Wafunguka Tetesi za Kumsajili Ntibanzokiza ‘Saido’, Watangaza Mipango Mipya-Michezoni leo

Mrundi, Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’.

 

BAADA tetesi nyingi kuzagaa za kiungo Mrundi, Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ kutua Simba, uongozi wa timu hiyo umeibuka na kutamka hauna mpango wa kumsajili.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu Yanga itangaze kutomuongezea mkataba kiungo uliomalizika Juni 30, mwaka huu.

 

Mmoja wa mabosi wa Simba, ameliambia Spoti Xtra kuwa, ngumu kwao kumsajili mchezaji ambaye ameachwa na timu yake kutokana na utovu wa nidhamu.

 

Bosi huyo alisema, sababu nyingine ni umri na majeraha ambayo yanamuandama mchezaji huyo kila wakati akiwa Yanga kabla ya kutangaza kuachana naye.

 

Aliongeza kuwa, Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, imepanga kufanya usajili bora na kabambe kujiandaa na msimu ujao, huku wakiwa katika mipango ya kukisuka kikosi kuwa imara kitakachoundwa na vijana wengi.

 

“Hizo tetesi tumeanza kuzisikia mara baada ya kiungo huyo kuachana na Yanga, hakuna ukweli wowote katika hilo, Simba hatuna mpango na Saido.

 

“Mchezaji aliyeshindikana na timu nyingine kutokana na tatizo la kinidhamu aje kusajiliwa Simba kwa sasa ni ngumu, kama uongozi tuna malengo makubwa.

 

“Malengo yetu ni kufika hatua ya nusu fainali au fainali ya michuano ya kimataifa, hivyo ni lazima tuwe na kikosi imara kitakachofanya vizuri msimu ujao,” alisema bosi huyo.

 

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alizungumzia usajili wa timu hiyo kwa kusema: “Tuna malengo makubwa na timu yetu kuelekea msimu ujao, tumepanga kufanya usajili mkubwa utakaotupa makombe, hivyo tusubiri muda ufike tuweke wazi.”

STORI: WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA

HUZUNI YANGA, Wachezaji 14 WAACHWA, MO DEWJI Atenga MAMILIONI ya USAJILI SIMBA | KROSI DONGO

The post Simba Wafunguka Tetesi za Kumsajili Ntibanzokiza ‘Saido’, Watangaza Mipango Mipya appeared first on Global Publishers.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz