Samaki mwenye uzani wa kilo 300 (lb 661) aliyevuliwa katika mto Mekong nchini Cambodia ndiye samaki mkubwa zaidi wa maji baridi kuwahi kurekodiwa, wanasayansi wanasema.
Samaki huyo (stingray) amempiku mwenye rekodi ya awali, samaki aina ya kambare mwenye uzito wa 646lb (293kg) aliyevuliwa nchini Thailand mwaka wa 2005.
"Katika miaka 20 ya kutafiti samaki wakubwa katika mito na maziwa katika mabara sita, huyu ndiye samaki mkubwa zaidi wa maji baridi ambaye tumewahi kukutana nao au ambaye amerekodiwa mahali popote ulimwenguni," Zeb Hogan, mwanabiolojia katika mradi wa uhifadhi unaofadhiliwa.
Hakuna uwekaji rekodi rasmi au hifadhidata ya samaki wakubwa zaidi wa maji baridi duniani.
"Kupata na kuweka kumbukumbu za samaki huyu ni jambo la kushangaza, na ni ishara chanya adimu ya matumaini, hata zaidi kwa sababu imetokea katika Mekong, mto ambao kwa sasa unakabiliwa na changamoto nyingi," aliongeza Dk Hogan.
Mradi wa uhifadhi unafanya kazi na Utawala wa Uvuvi wa Cambodia kuanzisha mtandao wa wavuvi ambao huwatahadharisha watafiti iwapo watakamata samaki wakubwa au walio hatarini kutoweka.
Stringray kubwa ya maji baridi ni spishi iliyo hatarini kutoweka. Huyu ni stingray wa pili kuchunguzwa na timu hiyo tangu Mei - yule wa awali alikuwa na uzito wa kilo 181.
No comments:
Post a Comment