Sababu za Ndege Kumwaga Mafuta Ikiwa Angani Kupitia Nozzle… Soma Hapa Kujifunza - EDUSPORTSTZ

Latest

Sababu za Ndege Kumwaga Mafuta Ikiwa Angani Kupitia Nozzle… Soma Hapa Kujifunza


Kunapotokea hitilafu yoyote ya ndege ikiwa angani, hususan ikiwa ni muda mfupi baada ya kuruka, rubani huwa hana uwezo wa kuishusha ndege na kutua mpaka afanye kitu kinachoitwa fuel dump au jetsoning, kitendo ambacho kwa lugha rahisi unaweza kukielezea kama ni kumwaga mafuta kutokea angani.


Kwa kawaida, kabla ndege haijapaa, hujazwa mafuta ambayo yatatumika katika safari husika, lakini pia huwa kuna kiwango kingine kikubwa cha mafuta ambacho huwekwa kama akiba, endapo ndege italazimika kukaa angani muda mrefu zaidi tofauti na ule uliotarajiwa.


Mafuta haya huwa na uzito wa tani nyingi. Kwa jinsi ndege ilivyotengenezwa, inao uwezo wa kuruka hata ikiwa na mzigo mzito lakini katika kutua, ni lazima uzito wa ndege upungue mpaka kufikia kiwango ambacho kitaalamu huitwa maximum landing weight.


Endapo ikitua na mzigo mzito, uwezekano mkubwa ni kwamba itatua kwa spidi kubwa kuliko kawaida, gia ya kutulia (landing gear) inaweza kupata hitilafu, magurudumu yanaweza kupasuka, injini zinaweza kulipuka na uharibifu mwingine unaoweza kusababisha ndege ikalipuka.


Kwa hiyo inapotokea dharura, rubani hu-activate kifaa maalum cha ‘jetson’ ambacho huruhusu mafuta kuanza kutoka kwa kupitia nozzle maalum zilizopo upande wa nyuma wa mabaya ya ndege, mbali na injini ili kuzuia mlipuko.


Rubani atapiga mahesabu ya kiwango anachotakiwa kukimwaga mpaka atakapofikia uzito ambao unamruhusu kutua, ambao huonekana kwenye dashboard ya ndege kulingana na mzigo na aina ya ndege. Baada ya hapo sasa, ndipo atakapoweza kutua kwa urahisi bila kusababisha hatari yoyote.


Zoezi hili hufanyika umbali mrefu kwenda juu ili kuyafanya mafuta yayeyushwe na hewa kabisa ili kuzuia athari kwa watu, wanyama na mazingira.


Lazima zoezi hili liongozwe na air controllers waliopo ardhini ambapo rubani huelekezwa njia ya kupita ili kuzuia ndege nyingine zisije zikapita eneo hilo na kulipuka.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz