Zari alipwa milioni 49.7(Ksh.2.5 milioni) kwa siku tatu za kikazi alizokuwepo nchini Kenya, na bado ilikuwa ngumu mrembo huyo kukubali dili hilo
Ambapo Kati ya hizo Ksh.800,000(Tsh.15.9 milioni) alilipwa kwa ajili ya kujitokeza(appearance) katika klabu ya XS millionaire palipokuwa na event ya All-White Party
Pia amelipwa milioni 1.7 za Kenya(Tsh.33.8 milioni) na kampuni ya Fine Urban Interiors inayojihusisha na ujenzi na upambaji wa majengo ili awatangazie biashara yao. Walimsafirisha Zari nchini humo atembelee majengo yao ya kifahari na achukuliwe picha na videos zitakazotumika katika promo kuitangaza kampuni hiyo
Lakini pamoja na mkunjwa huo mrefu aliolipwa ndani ya siku tatu alizokuwepo nchini humo kikazi bado mrembo huyo imeelezwa ilikuwa ngumu kumshawishi akubali dili hilo na hata kumlipia gharama afike Kenya haikuwa kitu rahisi kwa mujibu wa mmoja wa wahusika waliofanikisha dili hilo
Licha ya mama huyo wa watoto 5 kulipwa pesa hizo lakini ilibidi arudishe kiasi kingine cha pesa Ksh.200,000(Tsh.3.9 milioni) alizokuwa ameshalipwa na kampuni nyingine inayojihusisha na mambo ya utalii ambapo awali walitaka wamsafirishe Zari kwa gharama zao akale maraha mbugani kisha atumie picha husika na video kuwapa promo kampuni husika ila alijitoa katika dili hilo hatua za mwisho hivyo akawarudishia pesa zao
Zari aliambatana na boyfriend wake mpya na kupotezea kuonana na Diamond Platnumz aliyengia Nairobi kikazi siku moja baada ya Zari, Diamond alifika nchini humo kikazi baada ya kuingia mkataba na kampuni ya nchini humo kuhusu WasafiBet kila mmoja alilala hotel yake na hawakuonana
No comments:
Post a Comment