Nandy na Billnass Watarajiwa Kufunga Ndoa Mwezi huu wa Sita - EDUSPORTSTZ

Latest

Nandy na Billnass Watarajiwa Kufunga Ndoa Mwezi huu wa Sita
Faustina Charles au Nandy na Wiliam Lymo au Bilnass au Nenga; ni mastaa wakubwa wa muziki nchini Tanzania ambao hayawihayawi sasa yanaenda kuwa kwani ndoa yao ni mwezi huu.

Wawili hao wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu ambapo wamekuwa wakipita kwenye milima na mabonde na vipindi vya kupwa na kujaa kwa maji.


Nandy na Billnass Mapumzikoni
Hivi karibuni Nandy na Nenga walikwenda nchini Uturuki kwa ajili ya shopping ya gauni la harusi na suti kuonesha kwamba maandalizi yanaendelea.

Katika mahojiano na Gazeti la IJUMAA hivi karibuni, Nandy alisema ndoa yake hiyo itakuwa ni baab’kubwa kwani itafunga mitaa.


 
Kwa mujibu wa baba mzazi wa Nandy, Charles Mfinanga siku ile ya kuvishana pete ya uchumba, ndoa hiyo ilipangwa kufungwa Juni 25, 2022 (mwezi huu).
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz