Mwanamuziki wa Nigeria Osinachi Hatimaye Azikwa Mumewe Akikosa Kuhudhuria
Mwanamuziki Osinachi Nwachukwu alizikuwa alikozaliwa bila uwepo wa mumewe.
Mazishi hayo yalifanyika Isochi Umunneochi, mji ambao alizaliwa, bila uwepo wa mumewe ambaye anazuiliwa rumande kwa tuhuma za dhulma za nyumbani na kusababisha kifo cha msanii huyo, japo amezidi kukana.
Mtoto wa kwanza wa Osinachi, alisema kuwa baba yao Peter Nwachukwu, alikuwa akiwaambia kuwa kuwapiga na kuwatesa wanawake ni sehemu ya maisha.
Kwa mujibu wa mtoto huyo baba yao alizoea kumpiga marehemu hata kwa ugomvi mdogo tu na kwa wakati mmoja alimsukuma nje ya gari wakiwa safarini na kumwamuru arudi nyumbani.
Mumewe Osinachi kuendelea kuwa rumande
Kifo cha Osinachi kilichochea hasira kubwa ndani na nje ya Nigeria baada ya familia yake kudai kuwa alikuwa mwathiriwa wa dhulma za kindoa.
Mwaka 2017, Marehemu aliimba wimbo wa Injili uliovuma sana kwa jina Ekweume ambao umetazamwa mara milioni 77 kwenye mtandao wa video wa YouTube.
Baadhi ya mashtaka yanayomkabili Peter Nwachukwu hanahusiana na dhulma za kindoa kwa hisia, matamshi na akili pamoja na mauaji ambayo adhabu yake ni kifo.
Mahakama Kuu ya Abuja iliamuru Nwachukwu kuzuiliwa kwa rumande. Amekuwa rumande polisi wakiendelea kuchunguza kiini cha kifo cha mwanamuziki huyo.
Ripoti za awali zilisema kuwa Osinachi aliyefariki akiwa na umri wa miaka 42, alikuwa akiugua saratani ya koo lakini familia yake ilipinga madai hayo.
No comments:
Post a Comment