Mwanamke Mmarekani amekiri kuongoza batalioni ya wanawake pekee ya wanawake wa kile kinachoitwa kikundi cha Islamic State nchini Syria, pamoja kupanga njama za mashambulizi katika ardhi ya Marekani.
Allison Fluke-Ekren alikiri shitaka moja la kutoa usaidizi kwa kikundi hicho na akakiri kwamba alitoa mafunzo kwa wanawake na wasichana yatakayowawezesha kufanya mashambulizi.
Mama na mwalimu aligeuka kuwa kiongozi wa IS na kuondoka nchini Marekani katika mwaka 2011, na kufanya kazi na kikundi hicho cha ugaidi katika taifa la Libya kabla ya kwenda Syria.
Anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 20 jela kutokana na hukumu iliyotolewa katika mwezi Oktoba.
Fluke-Ekren, mwenye umri wa miaka 42, ambaye alikuwa mwanafunzi wa zamani wa baiolojia na mwalimu, alisafiri kwenda Syria kujiunga na kikundi hicho baada ya kuishi Misri na Uturuki.
Alipokuwa katika IS, aliongoza bataliani yawanawake pekee inayofahamika kama Khatiba Nusaybah, yenye makao yake katika mji wa Raqqa, nchini Syria.
Kazi yake kuu ilikuwa ni kuwafundisha wanawake na Watoto kutumia silaha, kama vile bunduki ya AK-47 , gurunedi na kutumia fulana za kujilipua, kulingana na maafisa
No comments:
Post a Comment