Mrembo Afariki Akifanyiwa Sajari ya Kuuboresha Mwili Wake Lagos, Nigeria - EDUSPORTSTZ

Latest

Mrembo Afariki Akifanyiwa Sajari ya Kuuboresha Mwili Wake Lagos, Nigeria



Crystabel; ni mrembo slay queen maarufu jijini Lagos nchini Nigeria ambaye anadaiwa kufa hospitalini alikokuwa amekwenda kufanya sajari ya kuuboresha mwili wake (plastic surgery) uwe na mwonekano unaovutia zaidi.

 

Rafiki wa mrembo huyo, Posha anasema; “Nataka kueleza hadharani, rafiki yangu alifariki dunia katika hospitali Lagos, Nigeria, siku chache zilizopita. ambapo alifanyiwa upasuaji.

“Sasa mimi sipingani na mtu yeyote anayetaka kuongeza mwili wake au kitu chochote kama hicho, ni maisha yako ya mwili na ni chaguo lako, kwa hiyo fanya kile unachopenda, lakini ninapingana na madaktari wanaodai kuwa wana uzoefu kutoka nje ya nchi, wamekuja Nigeria kuua vijana wa watu.


“Baada ya upasuaji rafiki yangu alilalamika kutokwa na damu na madaktari walidai ni kawaida, itakoma. Sasa tatizo ni hili, vipi wewe ni daktari bingwa wa plastic surgery mwenye ujuzi wa hali ya juu na mwenye uzoefu kutoka nje ya nchi na ukimaliza kumfanyia upasuaji mtu akalalamika damu ukasema ni kawaida itakoma?

“Hospitali haikuona umuhimu wa kuwasiliana na jamaa yake yeyote mpaka marafiki wachache waliojua anakwenda kufanyiwa upasuaji waliposema alitakiwa kuwa amerudi, waliamua kwenda hospitali kumchungulia; walipofika, walipewa barua kwamba mwili wake umewekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. Hii inasikitisha.”




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz