Mcheza Mpira wa Kike Clara Aliyedhaniwa ni Mwanaume Afunguka "Mimi ni mwanamke napiga kazi" - EDUSPORTSTZ

Latest

Mcheza Mpira wa Kike Clara Aliyedhaniwa ni Mwanaume Afunguka "Mimi ni mwanamke napiga kazi"



Clara Luvanga ni kati ya wachezaji walioonyesha mchango mkubwa wa kuisaidia timu hiyo kufuzu kucheza michuano ya Dunia, itakayofanyia nchini India 2022.

Amejibu swali la wanahabari waliomuuliza anachukulia mashabiki wanapomuona kama mwanaume? Amejibu "Naona ni moja ya njia ya mafanikio yangu, najijua ni mwanamke hizo nyingine ni changamoto tu.

Ameongeza "Wakati tulivyokwenda Cameroon walinikagua wakanikuta mimi ni mwanamke, sikutaka kuliweka hilo akilini maana lingeweza kuniondoa kwenye ari ya mchezo, nilichukua kama changamoto ya kupita na imepita," amesema.

Amesema hawezi kukata tamaa kuipambania ndoto yake ya kuwa mchezaji ndani na nje, hivyo hana budi kuziweka mbali changamoto zenye chembechembe za kuharibu anachokipigania.
Clara mwenye mabao 10 kwenye michuano hiyo, amesisitiza wachezaji wengine wanaopitia kwenye changamoto kama yake waangalie kazi, mengine wayaache kama yalivyo.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz