Jeshi la Polisi Mkoani Mara linamshikilia Gimusi Murimi (42), Mkazi wa Wilaya ya Serengeti kwa madai ya kumjeruhi mkewe kwa kumuingizia panga sehemu za siri akimtuhumu kuchepuka
Kamanda wa Polisi Mara, Longinus Tibishubwamu amesema Mtuhumiwa anafanya kazi Katoro, Geita na Mei 25, 2022 aliporejea nyumbani alibaini mkewe sio mwaminifu kwenye ndoa
Kamanda anasema "Akamshambulia kwa fimbo na baadaye kumwingizia panga sehemu za siri na kumuumiza sana. Mwathirika yupo hospitali akipatiwa matibabu, uchunguzi unaendelea huku mtuhumiwa tukiwa tumemshikilia"
Tukio hilo ni mwendelezo wa matukio ya migogoro katika mahusiano. Je, Sheria kali na ushauri toka Wataalamu wa Saikolojia (Psychology) na Viongozi wa Dini vinaweza kubadili hali hii?
No comments:
Post a Comment