Mwanaume huyo alijitambulisha kwa jina la Viktor Muller Ferreira na alikuwa ametuma maombi ya mafunzo ya kazi bila malipo katika taasisi hiyo, yenye jukumu la kuchunguza, miongoni mwa mashtaka mengine, uhalifu wa kivita unaowezekana uliofanywa katika Vita vya Ukraine.
Alifukuzwa nchini Brazil na, kulingana na PF (Polisi wa Shirikisho), yuko kizuizini na atafunguliwa mashtaka kwa makosa ya kutumia hati za uwongo.
Mamlaka ya Uholanzi inasema jina lake halisi ni Sergey Vladimirovich Cherkasov na yeye ni jasusi wa GRU - jasusi wa kijeshi wa Urusi.
Taasisi ya Ujasusi na Usalama Uholanzi (AIVD) iliripoti kwamba ikiwa ameweza kuchukua na kuingilia shirika, angeweza kufanya madhara makubwa.
"Tishio linalosababishwa na afisa huyu wa ujasusi linachukuliwa kuwa linaweza kuwa kubwa," shirika hilo lilisema katika taarifa.
Kwa wale waliomfahamu, Viktor Muller Ferreira alikuwa Mbrazil aliyependa masuala ya kimataifa. Lakini kwa kweli, AIVD ilisema, yeye ni aina fulani ya jasusi wa Kirusi anayejulikana kama "haramu".
Hivi ndivyo ujasusi wa Urusi unavyowatofautisha maafisa hawa na majasusi "wa kisheria" wanaojifanya wanadiplomasia. Nchi nyingi hutumia wapelelezi wanaojifanya kuwa watu wa kawaida, lakini kwa muda mrefu Urusi imebobea katika aina ya uwakala haramu wa siri ambao huchukua utaifa tofauti kabisa na wao.
Wapelelezi hawa wanajifanya kuwa Wamarekani, Waingereza, Wacanada au katika kisa cha Ferreira, Wabrazili ili kuwaruhusu wasogee katika duru ambazo Warusi wangetiliwa shaka na kwa hiyo wangekuwa na ugumu zaidi wa kufanya kazi.
AIVD ilichapisha hati inayoaminika kuwa imeandikwa na Cherkasov mwaka 2010, ambayo anaelezea utambulisho wake wa uwongo, labda kumsaidia kujificha kwake.
Makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu yanapatikana The Hague, Uholanzi
Chanzo cha picha, Reuters
"Mimi ni Viktor Muller Ferreira", anaanza.
Ugunduzi wa hati hiyo unaonesha kiwango cha ajabu cha uzembe wa upande wa jasusi.
Zaidi ya kurasa nne, anazungumza kuhusu historia ya familia yake. Anasema alizaliwa Aprili 4, 1989, huko Niterói (RJ) na aliishi nje ya nchi kwa miaka mingi na shangazi, baada ya mama yake kufariki kwa homa ya mapafu. Asingekuwa na ufasaha wa Kireno, jambo ambalo linaweza kuonekana kwa makosa ya kisarufi yanayorudiwa.
Katika ripoti hiyo, mtu huyo anasema aliachwa na baba yake, alilelewa na mama yake, ambaye alijishughulisha na muziki. Alipougua, shangazi ambaye hakuishi Brazil alimchukua akaishi naye.
Kulingana na waraka huo, alipokuwa bado Brazil, anasema anakumbuka daraja la Rais Costa e Silva, linalojulikana kama Rio-Niterói, na kwa hivyo alichukia harufu ya samaki.
Baada ya kifo cha shangazi yake, alimtafuta baba yake huko Rio de Janeiro na, ingawa walikutana, alikatishwa tamaa na mazungumzo waliyokuwa nayo.
Kutoka hapo, anasema alienda Brasília, ambako "sambamba na kurejeshwa kwa uraia" alikuwa na masomo ya binafsi ya Kireno. Kuhusu mji mkuu, anaorodhesha maeneo ambayo alipenda kwenda, kama vile mgahawa wa A Tribo - ambao upo. "Mkahawa huu unatengeneza chakula cha mchuzi wenye maharage na nyama kiitwacho feijoada bora zaidi mjini."
"Baba yangu alikuwa mtu wa urafiki na muwazi sana, lakini kwa mshangao niligundua kwamba nilimlaumu kwa vifo vya mama na shangazi na taabu na fedheha zote nilizopata katika maisha yangu," inasomeka sehemu ya waraka huo.
Shirika la usalama la Uholanzi AIVD lilisema iwapo jasusi huyo angefanikiwa kujipenyeza katika mahakama ya ICC, angeweza kufanya uharibifu mkubwa
Chanzo cha picha, Getty Images
Inaweza kuchukua miaka mitano hadi 10 kwa jasusi haramu kujifunza na kujenga maficho yake. Kwa kuzingatia changamoto, inaaminika kuwa sio wengi wanaokuwa kwenye operesheni - labda chini ya watu 30 wa taasisi ya GRU, kulingana na makadirio ya Magharibi.
Mahakama ya ICC kwa muda mrefu imekuwa ikilengwa na ujasusi wa Urusi, na inaaminika Ferreira alianza kuhama ili kupata taaluma katika taasisi hiyo mwishoni mwa mwaka jana. Umuhimu wa mahakama hiyo umeongezeka tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake nchini Ukraine. Mnamo Machi 3, mwendesha mashtaka wa ICC alifungua uchunguzi kuhusu uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu nchini Ukraine.
ICC inatoa karibu mafunzo 200 ambayo hayajalipwa ambayo yanawapa watahiniwa fursa ya "kupata kufichua mazingira ya kazi ya kila siku ya ICC na kuweka ujuzi na uzoefu wao katika vitendo chini ya usimamizi wa wataalamu".
Nafasi hiyo ingempa ufikiaji wa habari muhimu.
"Ikiwa afisa wa ujasusi angeweza kuanza kufanya kazi na ICC, angeweza kukusanya taarifa za kijasusi na kutafuta (au kuajiri) vyanzo na kutoa ufikiaji wa mifumo ya kidigitali ya ICC," AIVD ilisema katika taarifa.
"Kwa njia hii, anaweza kutoa mchango mkubwa katika ujasusi ambao GRU inatafuta. Anaweza pia kuwa na uwezo wa kushawishi mashtaka ya jinai ya ICC."
Kuomba wadhifa katika ICC ilikuwa hatari kwa jasusi wa siri, lakini wakubwa wake huko Moscow lazima walifikiri ilikuwa ya thamani yake. "Haramu" ni vigumu kupata - utambulisho wake halisi unaaminika kuwa haujagunduliwa na ICC - na mamlaka ya Uholanzi haijasema jinsi alivyotambuliwa.
Taarifa zake za mitandao ya kijamii zilizochambuliwa na BBC na kuaminiwa kuwa za Ferreira zinaonesha orodha ndefu ya marafiki - ikiwa ni pamoja na wanafunzi kadhaa wa kimataifa kutoka taasisi mbili anazoonekana kuwa alisoma - Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani na Chuo cha Trinity huko Dublin, Ireland.
Mara baada ya kuhitimu, marafiki hawa waliendelea kufanya kazi katika maeneo tofauti, kutoka benki ya uwekezaji Goldman Sachs hadi shirika la Think Tank na mashirika ya udhibiti huko Washington DC. Hakuna dalili kwamba walijua mtu huyo alikuwa jasusi wa Urusi.
"Alikuwa na lafudhi ambayo sikuweza kuitambua. Lakini haikuwa Kirusi," mmoja wa walimu wake aliiambia BBC. Ferreira anaaminika kuwa alituma maombi kwa ICC mnamo Septemba 2020, lakini uhakiki wa ombi hilo unaweza kuwa ulicheleweshwa kwa sababu ya janga la Covid-19.
Wasifu unasema Ferreira alihamia Washington D.C. mnamo Agosti 2018 na rekodi inaonesha alihitimu kutoka Chuo cha Johns Hopkins mnamo 2020.
Katika mojawapo ya machapisho hayo, alichapisha ripoti ya kikundi cha utafiti cha Bellingcat kuhusu ugunduzi wa vitambulisho mtandaoni vinavyotumiwa na GRU, hatua isiyo ya kawaida kwa mtu ambaye sasa anashutumiwa kuwa wakala wa siri wa GRU.
Hata hivyo, baada ya jalada lake kupeperushwa, maisha yake ya baadaye kama jasusi wa siri yatakwisha.
No comments:
Post a Comment