MCHAKATO wa uchaguzi ndani ya Klabu ya Yanga, umezidi kushika kasi ambapo jana Jumamosi orodha ya majina ya wagombea yaliwekwa wazi kwa waliopitishwa na wasiopitishwa.
Upande wa wagombea nafasi ya urais, jina la Injinia Hersi Ally Said limebaki peke yake, huku makamu wa rais wakiwa ni Arafat Haji na Suma Mwaitenda.
Kwa upande wa wajumbe, waliopitishwa ni Said Baraka Kambi, Salum Bakari Mkemi, Gerrad John Kihinga, Saady Mohamed Khimji, Semi Yusuph Semi, Seif Khamis Gulamali, Munir Said Seleman, Issa Ali Abas Mangungu, Wilbard Rutaremwa Kilenzi, Salim Seif Rupia, Sylvester Bernard Haule, Leevan Spanish Maro, Omary Hassan Kimosa, Edgar William Chibura, Philipo Winsper Haule Alexander Francis Ngai, Dominick Albinus, Benjamin Jackson Mwakasonda, Rogers Gumbo, Yanga Evans Makaga, Samwel Charles Lukumay na Hussein David Nyika.
Ikumbukwe kuwa, Julai 10, mwaka huu, Yanga inatarajiwa kufanya Mkutano Mkuu maalum wa uchaguzi uliopangwa kufanyika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Julius Kambarage Nyerere, Dar, ukiwa na ajenda kuu tatu.
Ajenda hizo ni; 1. ufunguzi wa kikao, 2. Kufanyika kwa uchaguzi wa nafasi zinazoshindaniwa, 3. Kufunga na mwisho wa mkutano.
USAJILI wa AZIZ KI; “MO DEWJI AMEWEKA FEDHA za KUTOSHA, MSIPOTOSHWE” – AHMED ALLY
The post Injinia Hersi Abaki Peke Yake Urais Yanga, Uchaguzi Julai 10, Wagombea Wote Wapo Hapa appeared first on Global Publishers.
No comments:
Post a Comment