Huzuni, Wachezaji 14 Ndani ya Kikosi cha Yanga Kufyekwa Msimu Ujao wa 2022/23 -Video-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Huzuni, Wachezaji 14 Ndani ya Kikosi cha Yanga Kufyekwa Msimu Ujao wa 2022/23 -Video-Michezoni leo

 

Heritier Makambo

 

MASTAA 14 ndani ya kikosi cha Yanga, wapo kwenye hesabu za kufyekwa kwa ajili ya kukiboresha kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa 2022/23.

 

Msemaji wa Yanga, Haji Manara, aliliambia Spoti Xtra kuwa, usajili wa msimu ujao utakuwa ni mkubwa na wenye kuzingatia ripoti ya benchi la ufundi.

 

“Tuna malengo makubwa na tunajua wapi ambapo tulishindwa msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, sasa tutasajili wachezaji wazuri na wenye uwezo mkubwa ili kuleta ushindani kimataifa,” alisema Manara.

 

Dennis Nkane

 

Habari zinaeleza kuwa, miongoni mwa wachezaji ambao wataachwa moja kwa moja na wengine kutolewa kwa mkopo ni Erick Johore na Ramadhan Kabwili, hawa ni makipa hawajacheza hata mechi moja ya ligi msimu huu.

 

David Bryson, amecheza mechi 6, Abdallah Shaibu (mechi 1), Deus Kaseke (mechi 10) na Heritier Makambo (mechi 18), Yusuph Athuman (mechi 6), Yassin Mustapha (mechi 9), Paul Godfrey (mechi 1), Crispin Ngushi (mechi 3), Dennis Nkane (mechi 10), Balama Mapinduzi (mechi 1), Chico Ushindi (mechi 5) na Ibrahim Abdallah (mechi 2).

LUNYAMADZO MLYUKA

The post Huzuni, Wachezaji 14 Ndani ya Kikosi cha Yanga Kufyekwa Msimu Ujao wa 2022/23 -Video appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz