Hivi ndivyo mabilioni yanaliwa halmashauri - EDUSPORTSTZ

Latest

Hivi ndivyo mabilioni yanaliwa halmashauri



 
MBUNGE wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo, ameitaka serikali kuzibana halmshauri ambazo zina matumizi makubwa kiasi cha kufikia hatua viongozi wake kugawana fedha kwenye akaunti zao binafsi na kununua magari.

Akichangia mjadala wa mapendekeo ya bajeti ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha bungeni jana, Gambo alisema ni lazima serikali inapobana matumizi, kuangalia fedha za matumizi kwa baadhi ya halmashauri ambazo zinaonekana kutapanya.

Alisema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam lina makadirio ya Sh. bilioni 81 zikijumuisha mapato ambayo aliyoyaita yasiyolindwa Sh. bilioni 62.2 a ikitolewa asilimia 70 ya maendeleo ambayo ni Sh. 43.587, Sh. bilioni 18 ni kwa ajili ya matumizi mengine kama posho na mafuta.

Gambo alisema kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma makisio ya mapato ni Sh. bilioni 55, mapato yasiyolindwa ni Sh. bilioni 44, inayokwenda kwenye maendeleo asilimia 60 ni Sh. bilioni 26 huku matumizi ya kawaida Sh. bilioni 17.

Alisema Halmashauri ya Kinondoni makisio yake ni Sh. bilioni 57 na mapato yasiyolindwa ni Sh. bilioni 46, matumizi ya maendeleo ni Sh. bilioni 32 na hivyo kuwa na matumizi ya kawaida Sh. bilioni 14.


 
Mbunge huyo alisema Halmashauri ya Arusha makisio yake ni Sh. bilioni 30, mapato yasiyolindwa Sh. bilioni 24, asilimia 70 ya maendeleo ni Sh. bilioni 17 na matumizi ya kawaida ni Sh. bilioni saba.

“Tumeona mfano mmoja Jiji la Arusha kwa mapato ya Sh. bilioni saba wameingiziana fedha kwenye akaunti zao binafsi.

“Ushari wangu tunaomba Wizara ya Fedha na Mipango wakae na TAMISEMI badala ya kusema waangalie asilimia, waangalie matumizi halisi,” alisema.


Kwa mujibu wa Gambo, matumizi ya Halmashauri ya Dar es Salaam pekee ni sawa na ya halmashauri ndogo 14 ambazo matumizi ya kawaida kwa mwaka Sh. bilioni 9.9.

“Mimi nadhani kuna haja ya serikali kuangalia matumizi kwenye halmashauri, Rais anatafuta hela dunia nzima, anabana matumizi lakini Waziri wa Fedha na TAMISEMI msaidieni Arusha," alisema.

Alisema kwa Jiji la Arusha wanavyokula fedha, wakipewa Sh. bilioni tatu au nne zinawatosha na inayobakia ikajenge barabara, vituo vya afya na kupeleka huduma kwa wananchi.

Mbunge wa Kibamba, Issa Mtemvu, alitaka kuwe na viwango tofauti vya posho kwa madiwani kulingana na uwezo wa halmashauri kwa kuwa uwezo unatofautiana kutoka halmashauri moja hadi nyingine kukusanya fedha.

MIAMALA YA SIMU

Mbunge wa Manyoni Mashariki, Dk. Pius Chaya, alitaka serikali kuwasilisha bungeni tathimini ya kodi ya miamala ya simu na ukusanyaji wa kodi ya majengo kupitia Luku.

“Sijasikia katika taarifa yako ukisema kwa kwango gani tumefanikiwa kwenye vyanzo hivi, kwamba tunaweza kuendelea na miamkala au kodi ya majengo kupitia luku,”alisema.

Kuhusu namba ya mlipa kodi, alisema ni wazo jema lakini serikali inapaswa kuondoa utitiri wa vitambulisho na kuwa kama nchi zingine ambazo mtoto anapozaliwa anapewa namba.






Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz