Global FC na Bongo Muvi Zatoshana Nguvu kwenye Mchezo wa Kirafiki-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Global FC na Bongo Muvi Zatoshana Nguvu kwenye Mchezo wa Kirafiki-Michezoni leo

Kikosi cha Global FC

ILE timu ghali Bongo ya Global FC inayomilikiwa na Kampuni ya Global Group iliweza kuonyesha ubabe wake mbele ya timu ya Bongo Movies kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Shule ya Msingi Muhimbili jana.

 

Kwenye mchezo huo wa kukata na shoka timu zote mbili zilicheza mchezo mkubwa ambapo Global FC walianza kupata bao la kuongoza kwa shuti kali la Mbwana Junior kwa pasi ya beki katili Omary Mdose ambaye ilikuwa ngumu kumpita.

 

Iliwabidi Bongo Movies wacheze muvi ya kweli kwa kufunga bao la kusawazisha kwa penati ya maajabu iliyofungwa na staa wao Idrisa Makupa iliyomshinda kipa namba tatu wa Global FC, Issa Liponda, ‘Mbuzi’.

Kikosi cha Bongo Muvi

Kijiji kizima cha mastaa wa Bongo Movie walijitokeza kushuhudia mchezo huo ambao ulikuwa ni wa aina yake ikiwa ni pamoja na mzee Chilo.

Nahodha wa Global FC,Wilbert Moland aliweza kutuliza presha ya wachezaji wa Global FC ambao walikuwa kwenye kasi kubwa kuwaandama Bongo Muvi.

 

Mbali na mchezo huo pia Bongo Movie walikuwa na timu ya mpira wa mikono ambapo huko waliibuka mashujaa kwa ushindi wa mabao 10-1 Global FC.

 

 

The post Global FC na Bongo Muvi Zatoshana Nguvu kwenye Mchezo wa Kirafiki appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz