Supastaa Diamondplatnumz anaendelea kutunisha misuli Kimataifa akiiwakilisha vyema Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kwenye orodha ya wasanii 10 toka Afrika wenye ushawishi mkubwa ulimwenguni.
Jina la Diamond linashika namba 4 kwenye orodha hiyo ambapo nafasi nyingi zikitawaliwa na wasanii wa NIGERIA.
Aidha boss huyo wa WCB, kupitia insta story yake ame-share orodha hiyo na kueleza kwamba siku akiondoka duniani, basi bendera ya Tanzania itaacha kupepea kwenye anga la Kimataifa Kimuziki katika top 10, pengine labda top 100.
"Kiufupi ikitokea nimekufa 🇹🇿 haipo hapo. Pengine top 100 inshallah 🙏" - ameandika Diamond Platnumz.
No comments:
Post a Comment